Pages

Thursday, February 28, 2013

CHRIS BROWN AJUTA KUMPIGA RIHANNA


LOS ANGELES, MAREKANI
CHRIS BROWN amesema kitendo chake cha kumpiga Rihanna ni kosa baya zaidi alilowahi kulifanya katika maisha yake, na kuongeza kuwa bado mwanadada huyo anampenda.
Staa huyo wa R & B - ambaye bado yupo kwenye kipindi cha uangalizi kutokana na shambulio alilofanya mwaka 2009 dhidi ya Rihanna anayetamba na kibao chake ‘Diamonds’, amedai kuwa sasa ni mtu aliyebadilika.
Alisema: “Wakati mwingine unagombana, unapigana na mtu unayempenda… Usiku ule ni wa majuto makubwa katika maisha yangu, kosa kubwa. Lakini ananipenda — ninaweza kusema nini? Mimi ni wa kusamehewa… lakini, ndiyo, ninafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya hilo.”
Wawili hao ambao walijitenga baada ya tukio hilo, sasa wamerudi tena kuwa pamoja, na Chris, mwenye umri wa miaka 23, anasisitiza kuwa amejifunza kutokana na makosa yake na kwamba hataweza kumuumiza tena Rihanna.

No comments:

Post a Comment