Pages

Thursday, February 28, 2013

MTOTO ABAKWA NA MJOMBA WAKE!!

Mkoani Geita Mtoto ambaye jina lake limehifadhiwa mwenye umri wa miaka 9 anaishi na Bibi yake baada ya wazazi kutengana amefanyiwa kitendo cha kikatili na cha udhalilishaji kwa kubakwa na mjomba wake na akimaliza kumbaka humwita rafiki yake ambaye nae humbaka wakati huo huo.

Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa pili katika shule ya msingi Geita amesema amekuwa akifanyiwa vitendo hivyo mara kwa mara kabla ya kwenda shule licha ya kukataa mjomba wake humpiga na hata alipotoa taarifa kwa bibi,bibi alimwita na kumkanya kuacha lakini kijana huyo aliendelea kumbaka.

Tatizo la mtoto huyo limejulika shuleni hasa baada ya kuwa anachelewa shule na maendeleo kuwa mabaya huku wakati mwingi akitumia kwenda msalani kujisaidia hali iliyowalazimu waalimu kumuhoji na ndipo kugundua unyama huo.

No comments:

Post a Comment