Pages

Tuesday, March 26, 2013

Diamond Platinum amsaidia Madee kumsaka aliyemwaga pombe yake

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’, anatarajiwa kuwa mmoja wa wasanii ambao wataonekana katika video ya wimbo wa ‘Nani kamwaga pombe yangu’ ulioimbwa na mkali wa muziki huo, Ahmed Ally ‘Madee’.

Video hiyo imeanza kutengenezwa Machi 19 jijini Dar es Salaam chini ya mtayarishaji mahiri, Adamu Juma.Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Madee aliwaomba mashabiki wake, wakae mkao wa kula kwa ajili ya kuipokea kazi hiyo, ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni.

“Nimeamua kumuomba Diamond aonekane katika video yangu, kutokana na kuwa na mashabiki wengi ambao wanamkubali, hivyo naamini uwepo wake, utanifanya nijizolee mashabiki lukuki kupitia video hii,” alisema mkali huyo ambaye pia ni kiongozi wa kundi la Tip Top Connection lenye maskani yake Manzese jijini Dar es Salaam.

Madee alisema mbali na Diamond, wasanii wengine ambao wataonekana katika video hiyo ni Albert Mangwea ‘Ngwea’ na Sharrif Thabit ‘Darasa’ ambao pia watanogesha kibao hicho.
Mbali na kibao hicho, Madee alishawahi kutesa na vibao vyake kama ‘Pesa’, ‘This is my Story’, ‘Siyo mimi’, ‘Nisikilize mimi’, ‘Napeleka benki’ na nyinginezo.

No comments:

Post a Comment