IMANI MAKONGORO
BONDIA wa Tanzania, Alphonce Mchumiatumbo ametangaziwa zali la
kucheza na Evander Holyfield wa Marekani, lakini mwenyewe anabainisha
tangu alipoambiwa anajifua usiku na mchana kumkabili mkali huyo wa
dunia.
Mchumiatumbo bondia namba moja kwenye uzani wa juu hapa nchini
ameeleza kuwa siku ya bambino hilo ataonyesha uwezo wake wote hadi ule
wa ziada kwani hiyo ndiyo nafasi ya yeye kutoka.
"Nimepewa taarifa kuwa Evander anakuja Tanzania Julai mwaka huu kama
kutalii lakini pia atacheza pambano moja, na mimi ndiyo nitacheza naye,
ni pambano la kuhamasisha ngumi hapa nchini," alisema Mchumiatumbo
katika mahojiano na Mwanaspoti.
Mchumiatumbo anabainisha kuwa kuna promota kutoka Marekani
aliyemtaja kwa jina la Jorge alimfuata baada ya pambano lake na Joseph
Marwa na kumwambia ajiandae atacheza na Evander.
"Kwa maelezo ya promota huyo Evandar ameshuka kiuchumi siyo yule wa
enzi hizo wakati anampiga Mike 'Iron' Tyson' na sasa ameamua kuja
Tanzania kutalii," alibainisha bondia huyo.
"Unajua ni kama zali tangu promota huyo aliponitaka nijifue ili
nicheze na Evander, muda mwingi nafanya mazoezi, najua litakuwa pambano
la kihistoria."
Rekodi zinaonyesha kuwa Evander ameshinda mara 44 (29 kwa KO),
amepigwa mara 10 (2 kwa KO), ametoka sare mara 2 wakati Mchumiatumbo
ameshinda mara 9 (8 kwa KO) hajawahi kupigwa ametoka sare mara moja.
No comments:
Post a Comment