Pages

Friday, March 1, 2013

FERGUSON ASEMA NJIA NYEUPE KUTWAA MATAJI MATATU MSIMU HUU

Alex Ferguson
LONDON, ENGLAND
ALEX FERGUSON amewatia mzuka nyota wake akiwaambia kuwa wana nafasi ya kuweka majina yao katika vitabu vya historia kwa kutwaa mataji matatu kwa mpigo ‘treble’ msimu huu.
Bosi huyo wa Old Trafford anaamini kuwa United inaweza kurudia mafanikio ya mwaka 1999 waliposhinda mataji ya Premier League, FA Cup na Champions League.

Ferguson amesema kuwa kilichopo kwenye akili ya wachezaji wake ni kwamba huu unaweza kuwa mwaka wa mafanikio makubwa kwao, na akaahidi kuwa wote watapata nafasi ya kutoa mchango wao wakati United ikifukuzia kurejea yaliyofanywa miaka 14 iliyopita.
“Wote walitaka kucheza dhidi ya Real na kulikuwa na wachezaji wengi walioangushwa (kwa kutocheza). Hilo lilikuwa zuri. Ni kipimo cha wanavyojiamini wenyewe,” alisema.
United inaongoza Premier League na bado imo kwenye kinyang’anyiro cha FA Cup, huku pia itacheza na Real Madrid katika mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya Champions League Jumanne ijayo.

No comments:

Post a Comment