Pages

Sunday, May 5, 2013

ARSENAL YAIFUNGA QUEENS PARK RANGERS 1-0, YATINGA TOP 4.

Washika bunduki wa London Arsenal wakicheza Ugenini kwa QPR Loftus Road Uwanja uliojengwa mwaka 1904, Bao la Theo Walcott la sekunde 20 tu baada ya kipenga cha Refa Jon Moss kupulizwa limewapa ushindi mtamu Arsenal na kupanda hadi nafasi ya tatu wakiwa na alama 67 chini ya Manchester City wenye Pointi 72 ambao pia leo wametoshana nguvu ya bila kufungana na timu ya Swansea City iliyopanda Daraja msimu huu unaomalizika hivi karibuni.

Ushindi huu pia unampa nafasi tena baada ya kutoka suruhu wiki iliyopita walipocheza na United. Ngoma inabaki kwa Chelsea ambao pia bado wanamichezo mingi na huku wakiwa na alama 65 sawa na Spurs wakipitwa na alama 2 tu, hivyo Arsenal bado wapo kwenye hali tete kwani timu hizo zikicheza na kupata ushindi zitamgoa Arsenal nafasi hiyo ya tatu.Arsenal sasa wamebakisha michezo 2 tu kufunga msimu huu na kujihakikishia nafasi ya kuwemo kwenye 4 bora ili kushiriki kombe la UEFA Champions.Gunners Pia wanabakiwa na mchezo nyumbani kati ya Wigan utakao chezwa tarehe 14 mwezi wa tano siku ya Jumanne saa 9:45 mchana na kisha kuelekea

Newcastle kucheza mchezo wa kumaliza msimu ambao utachezwa kwa muda mmoja na timu zote 20 za ligi kuu England, Mchezo utakao chezwa tarehe 19 mwezi huu wa tano tarehe 19 siku ya Jumapili saa 12:00 jioni.Theo Walcott naJi-Sung Park wakichuana vikali leo hiiArsene Wenger akiangalia vijana wake wakiminyana na timu kibonde inayoshuka daraja QPRTal Ben Haim na Aaron Ramsey wakigombania mpiraLoic Remyakimkingia kifua Aaron Ramsey wa ArsenalHapa hupiti:Theo Walcott na Stephane Mbia wakichuana Andros Townsend na Nacho Monreal wakikimbizana

No comments:

Post a Comment