BINTI mrembo aitwaye Flora Bahati Lyimo anamtuhumu mbunge mmoja ‘mtata’ wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloongozwa na Spika Anne Makinda.
BINTI
mrembo aitwaye Flora Bahati Lyimo anamtuhumu mbunge mmoja ‘mtata’ wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloongozwa na Spika Anne
Makinda (jina tunalo) kuwa amembaka, Uwazi lina kisa cha aibu ya karne. Katika uchunguzi wake, hivi karibuni gazeti hili lilielezwa kuwa kuna
habari ya kashfa nzito inayomtafuna mbunge huyo anayetokea Kanda ya
Kaskazini lakini haikufafanua kwamba inahusu nini.
VYANZO
Baada ya kutulia na kupekua kwenye vyanzo vyake, Uwazi lilibaini kuwa
kashfa inayomlenga mheshimiwa huyo ni ya ubakaji na tayari imefikishwa
mahakamani huko London nchini Uingereza. Habari hiyo ilielezwa
‘kijuujuu’ hivyo gazeti hili likamtafuta Flora ambaye ni Mtanzania
anayetokea mkoani Kilimanjaro ambaye anaishi katika Jiji la London
kikazi.
MAZITO Alipopatikana Flora alibanwa kisawasawa
ndipo akaibua mazito huku akieleza tukio zima lilivyofanyika kwa data na
vielelezo vya kila aina ikiwemo barua ya Mahakama ya Crown ya London.
“Ni kweli mheshimiwa … (anamtaja jina) alinibaka Agosti, mwaka jana.
Yeye na makada wenzake wa chama chake walikuja hapa London kwa ziara ya
kichama na kwa kuwa mimi sina chama nilikwenda kuhudhuria mkutano wao
kwa kuwa nina mtandao wangu (blog) hivyo nilitaka kupata habari za
kuingiza kwa sababu ni za watu wa nyumbani (Tanzania).
MAZOEA YAANZA
Akiendelea kuweka wazi kisa hicho, Flora anasema: “Nikiwa kwenye
mkutano….(jina la mbunge) alinifuata akaniuliza nimeandika watu wangapi
waliohudhuria mkutano huo, nikamjibu 50 akaniambia niongeze idadi hiyo
ili ionekane mkutano ulikuwa na watu (Watanzania waishio Uingereza)
wengi. “Hapo ndipo alipoanza kunizoea. Alitaka kunipa kadi ya chama
chake nikakataa, ndipo akadai kwamba mimi nilitumwa kwenye mkutano huo
na balozi na rais kwa ajili ya ushushushu.
KISA KUJISAIDIA HAJA NDOGO
“Mkutano ulimalizika, sasa nilipokuwa naondoka kurudi nyumbani kwangu,
mbunge huyo na wenzake nao walitoka. Tukiwa njiani wenzake walikwenda
kujisaidia haja ndogo, yeye akaniomba akajisaide nyumbani kwangu,
nilimkubalia. Alipofika ndani, bila kujua kila kitu kinaonekana kwenye
kamera alinibadilikia kama vile adui vitani, ona sasa wema wangu ukawa
umeniponza.
No comments:
Post a Comment