Pages

Sunday, May 5, 2013

BOMU LAKATISHA UZINDUZI WA KANISA LA MT. JOSEPH – OLASITI ARUSHA.

Habari na 2JIACHIE-  www.2jiachie.com

 
                                 Parokia mpya ya Mt. Joseph  iliyopo Olasiti jinni Arusha.
Parokia mpya ya Mt. Joseph  iliyopo Olasiti jinni Arusha imekumbwa na tukio kubwa ambalo si la kawaida kutokea katika makanisa,misikitini, na hata kuzoea hali hii katika maisha ya kawaida ya watanzania,
Tukio hilo lililotokea majira saa nne na dk kadhaa baada ya maandamano yaliyoanzia nje ya eneo la kanisa  yakielekea kanisani.
Baada ya kuingia eneo la kanisa kwa nje kabla ya kuingia ndani ya kanisa,  ndipo  palipotokea mlipuko wa bomu wakati  baba Askofu Francis Pandilla na balozi wa papa kutoka Vatican wakijiandaa kubariki maji ya Baraka ili wabariki waamini na kubariki kanisa hilo jipya kabla ya kuingia ndani ya kanisa na kuanza misa takatifu.
 
                                 Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akiwa eneo la tukio.
Huku waumini wa kanisa katoliki  nchini wakiwa makini kusikiliza Redio Maria  ambayo ndio iliyokuwa inarusha matangazo ya moja kwa moja  kutoka kanisani hapo  ilikatisha matangazo ya kawaida na kuanza kutangaza  tukio hilo live.
  
Huku watu wakiwa wemeshikwa na butwaa na kutojua maamuzi  ya haraka ya kufanya huku watoto wa maua hujulikana  kama  utoto wa yesu  wanaotanguliwa mbele  kupamba sherehe za wakatoliki  pamoja na vijana ndio waliokuwa waathirika zaidi wa tukio hilo.
Mwandishi  wetu alie kuwa eneo la tukio alishudia watu wakikimbia huku na huku kuokoa nafsi yake.
Mwandishi pia alishuhudia baadhi ya viongozi wa serikali waliopatwa na msituko. baada ya kupata taarifa ya mlipuko huo.
Mkuu wa mkoa wa Arusha akiwa njiani kuelekea eneo la tukio alikumbana na vikwazo njiani kutokana na wingi wa magari kuelekea eneo la tukio.
Viongozi hao akiwemo mkuu wa mkoa wa Arusha  Mh. Magesa Mulongo , Mh.Godbless Lema mbunge  wa jimbo la Arusha mjini, chadema  Mh. Joshua Nassari mbunge wa jimbo la Arumeru.
Mkuu wa wilaya  ya Arusha mjini Alitibua hali ya hewa pale pale alipowaambia waumini  pamoja na viongozi wa kanisa wa eneo la tukio kwa kusema. Tukio hili ni  la kawaida: waumini walionekana kuipokea  kwa mtazamo tofauti  kauli hiyo na kusababisha minong’ono ya hapa na pale kwa watu kutofarijika kwa maneno yake.
Mwandishi wetu aliondoka eneo la tukio na kuelekea Hosp ya ST ELIZABETH walikolazwa baadhi ya majeruhi , na kushuhudia baadhi ya majeruhi  wakiendelea  kupata huduma. 

Mwandishi wa 2jiachie akimpa pole mgonjwa.Alietoa baadhi ya maelezo hapo chini kwenye nukuu
Tuliongea na  na moja kati ya majeruhi hao  ambae alikuwa mbele kabisa na lilipotua bomu alisema yafuatayo:
  “ wakati tumesimama  tuu wakianza  kubariki maji, mimi nikaona kama jiwe limerushwa nikainama lisinipige wakati naendelea kuwauliza wenzangu mbona wanarusha mawe ghafla mlipuko, kumbe halikuwa jiwe ndio bomu lenyewe”
Pia mwandishi baada ya kutoka hapo alielekea hospital  ya Maunt  Meru  Ila hakupata nafasi ya kuingia  wodini kutokana wa kuzuiliwa kwa kutoa nafasi ya madaktari kutoa huduma ya haraka kwa majeruhi. Pamoja na kuongezewa damu majeruhi.
Mbunge wa Arusha mjini  Mh. Godbless Lema  Pia alijitolea Damu kwa kuwasaidia majeruhi.

moja kati ya kijana aliekuwa kwenye maandamano na kukutana na mlipuko. kama anavyoenekana amechafuka damu.
Hapa wana habari wa ITV wakiwa hewani eneo la tukio katika kanisa la Mt.Joseph Olasiti-Arusha.

Majeruhi waliolazwa katika hospitali ya ST. ELIZABETH  ARUSHA.
Gari ya Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema likiwa mbele ya eneo la hospitali ya Mount meru Arusha. Godbless Lema amejitolea damu siku ya leo kuwasadia majeruhi wa mlipuko wa bomu
 
Viongozi wa vijana wakatoliki jimbo la Arusha mjini wakiwa hospitali ya Mount Meru wakiwa tayari kuwafariji majeruhi kulia ni Sister mlezi wa vijana jimbo,John Masawe mwenyekiti jimbo na kulia ni Majegero Selecius mwana mipango wa kanda.



Habari na 2JIACHIE-  www.2jiachie.com

No comments:

Post a Comment