Pages

Wednesday, May 1, 2013

CHADEMA yailiza CCM Kilosa

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Kilosa kimeendeleza ubabe wa ushindi kwenye chaguzi ndogo baada ya juzi kunyakua viti vyote vya kitongoji na kijiji katika Kata ya Ruaha.

Uchaguzi huo ulifanyika kujaza nafasi hizo kutokana na waliokuwa wakizishikilia kufariki dunia na wengine kujuzulu.

Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi huo, Rashid Kalembela, nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Kifinga ilichukuliwa na Kilango Mshana aliyepata kura 451 na kumbwaga Castory Manga wa CCM aliyepata kuwa 248.

Katika Kitongoji cha Ruaha ‘B’, George Banda wa CHADEMA aliibuka mshindi kwa kura 428 dhidi ya Abdalah Kimbaa wa CCM aliyepata kura 155.
Akizungumzia ushindi huo, meneja kampeni wa wagombea wa CHADEMA, Mathew Likwina, alisema matokeo hayo yalilazimishwa kusomwa saa 12 jioni na umati wa watu baada ya kucheleweshwa makusudi.

Alisema mpango walionao sasa ni kuwaalika kwa gharama zao viongozi wa chama taifa kuja kushuhudia wanavyosimikwa na kutoa nasaha juu ya mfumo bora wenye tija katika kuongoza wananchi. 

No comments:

Post a Comment