MK/HB.VOL.6/013/1
06/05/2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAMKO LA BARAZA KUU LA WAISLAMU WA TANZANIA BAKWATA JUU YA MLIPUKO WA BOMU - ARUSHA
Assalaam alaykum warahmatullahi wabarakaatuh.
Baraza
Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA, limepokea kwa masikitiko makubwa
tukio la kurushwa bomu Kanisani na kusababisha upotevu wa maisha na
majeraha kwa watu wengi wakati wa sherehe ya uzinduzi wa jengo la Kanisa
la Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Orasiti, Arusha.
Kimsingi
hili ni jambo la kusikitisha, kukera na kufadhaisha sana kutokea hapa
nchini. Watanzania kwa miaka mingi, tumezoea hali ya utulivu na amani na
tukio kama hili ni changamoto kwa usalama wa Watanzania wote nchi nzima
Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA linalaani kitendo hicho cha
kikatili na inaviomba vyombo vya dola kufanya jitihada zote kuhakikisha
wahusika wanakamatwa na wanachukuliwa hatua, kwani msiba huu ni wetu
sote, Wakristo na Watanzania wote.
Kwa niaba ya Baraza Kuu la
Waislamu wa Tanzania mimi Sheikh Issa Bin Shaaban Simba Mufti wa
Tanzania nawapa pole wafiwa wote katika tukio hilo na kuwaombea dua
majeruhi na Mwenyezi Mungu (SW) awape tahfif na wapone haraka na kurudi
katika shughuli zao za kila siku.
Wabillahi Tawfiiq.
SHEIKH ISSA BIN SHAABAN SIMBA.
MUFTI NA SHEIKH MKUU WA TANZANIA BARA.
No comments:
Post a Comment