WATU 8 WATIWA MIKONONI MWA POLISI KUTOKANA NA TUKIO LA JANA HUKO ARUSHA.
Watu
wanane wakiwemo raia wa Saudi Arabia wamekamatwa nchini Tanzania,
kuhusiana na shambulio lililofanyika dhidi ya Kanisa moja wakati wa
ibada ya Jumapili jijini Arusha.
Tukio hilo la mripuko hadi sasa inasemekana watu watatu tayari wameuwawa na wengine kujeruhiwa.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ameliita shambulio hilo kuwa ni la
kigaidi, lililofanywa na mtu au kundi la watu wakatili, ambao ni maadui
wa nchi hiyo.
Watu wengine wasiopungua 30 walijeruhiwa katika shambulio hilo, ambalo ni la kwanza la ukubwa huo kulilenga kanisa.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amesema wasaudi wanne
waliokamatwa kuhusiana na shambulio hilo waliwasili katika uwanja wa
ndege wa Arusha siku ya Jumamosi, na kwamba Watanzania wanne
waliokamatwa ni wakristu, lakini hakutoa maelezo zaidi.
Balozi
wa Vatican nchini Tanzania Francisco Montecillo Padilla, alikuwa
akihudhuria misa katika kanisa hilo ambalo limejengwa upya, lililoko
katika viunga vya jiji la Arusha, lakini hakudhuriwa. Maafisa bado
hawajatoa ishara zozote kuhusiana na nani aliefanya shambulio hilo,
lakini wasiwasi umekuwa ukiongezeka kati ya jamii za Wakristu na
Waislamu katika miezi ya hivi karibuni. Aidha Rais Kikwete ametowa wito kwa raia wa Tanzania kuwa watulivu wakati polisi ikiendelea na uchunguzi wake.
No comments:
Post a Comment