Pages

Thursday, June 27, 2013

CHOKORAA, MCHUMBA’KE KIMENUKA.

MKURUGENZI wa Bendi ya Mapacha Watatu, Khaleed Chuma ‘Chokoraa’ (pichani), amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya mchumba wake aliyemtaja kwa jina  moja la Jessica kumcharukia na kumtaka waachane baada ya kunaswa akiwa na demu mwingine.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Chokoraa alisema tangu habari ya kunaswa na binti ‘mbichi’ aliyefahamika kwa jina la Lulu wakiingia kwenye Tuzo za Kilimanjaro zilizofanyika hivi karibuni, Mlimani City, mkewe alimjia juu na kumwambia waachane.
 
“Kiukweli hadi sasa sijajua muafaka wa mke wangu mtarajiwa, ninachofanya ni kuwatumia watu wamshauri ili aelewe kwamba yule binti hakuwa mtu wangu zaidi ya kukutana pale Mlimani City,” alisema Chokoraa.

No comments:

Post a Comment