Pages

Thursday, June 27, 2013

JACK PATRICK: MIMI SI WA KUZAA KESHO WALA KESHOKUTWA


MODO mwenye mvuto wa kipekee Bongo, Jacqueline Patrick (pichani) amefunguka kuwa baada ya kutemana na aliyekuwa mume wake, Abdullatif Fundikira hafikirii  kuzaa miaka ya hivi karibuni.
Akichonga na paparazi wetu juzikati jijini Dar, Jack alisema kwa sasa yeye na kuzaa mbalimbali kwa vile ana mipango mingi ya maisha ingawaje anapenda sana watoto.
 
“Napenda sana watoto lakini sitarajii kabisa kuzaa kesho wala keshokutwa, kwasababu ni lazima ujipange sawasawa ili uweze kumtunza vyema mtoto pindi utakapojifungua,” alisema na kuongea:
 
“Wanawake wengi wanaharakisha kuzaa matokeo yake ni kuwaacha watoto nyumbani na mahausigeli wakiwa wadogo ili wao wakatafute chochote,  lazima ukae na mwanao hata mwaka mmoja aweze kupata malezi bora ndiyo maana nasema lazima ujipange sana.”
Credit:GLP

No comments:

Post a Comment