Pages

Thursday, August 29, 2013

ASKOFU MOSES KULOLA AFARIKI DUNIA


 
Askofu Moses Kulola enzi za uhai wake.
Askofu Mkuu wa Kanisa la E.A.G.T na mhubiri wa kimataifa wa siku nyingi, Moses Kulola amefariki dunia. Askofu Moses Kulola amefariki leo.

Mtoto wa Askofu Kulola, ambaye naye pia ni mhubiri wa kimataifa na mchungaji wa kanisa la EAGT Lumala mpya,  Mch. Daniel Moses Kulola amethibitisha taarifa hizo kupitia katika akaunti yake ya Facebook. Kwa kuandika hivi: "WATU WA MUNGU SALAAM, NINA SALAAM ZA MAJONZI. BABA YANGU MZEE KULOLA AMEFARIKI MUDA SIYO MREFU."

Hivi karibuni  marehemu alilipotiwa kulazwa katika hospitali ya Bugando iliyopo mkoani Mwanza kwa matibabu kutokana na matatizo ya kiafya yaliyokuwa yanamkabili lakini Agosti 22 mwaka huu mwanaye Mch. Daniel Moses Kulola alieleza kuwa baba yake karuhusiwa  baada ya kupata nafuu.
MUNGU AILAZE ROHO YA ASKOFU KULOLA MAHALI PEMA PEPONI. AMEN

1 comment:

  1. Wana wa Mungu, tunasikitika katika hili mzee wetu amemaliza safari yake. Imefanya huduma ya Injili kwa kipindi chote cha maisha yake, alikuwa ni baba wa imani kwa watumishi wengi. Mungu aitie nguvu katika katika utumishi huu na pia familia kwa ujumla wake

    ReplyDelete