MCHEZAJI wa zamani wa Coastal Union ya Tanga, Idrisa Ngulungu amefariki dunia mapema leo.
Idirisa Ngulungu alitamba na Costal Union mwishoni mwa miaka ya themanini hadi mwanzoni mwa miaka ya tisini.
Alikuwepo kwenye kikosi kilichotwaa ubingwa wa Tanzania Bara mwaka 1988.
Kwa mujibu wa kaka wa marehemu, Hussein Ngulungu ambaye nae ni mchezaji
wa zamani wa Taifa Stars amesema Idrisa amefariki kwa ajali ya gari
iliyotokea eneo la Kisaki mkoani Morogoro.
Hussein Ngulungu
ameiambia Saluti5 kuwa Idrisa na ndugu wengine walikuwa wanaelekea
Kisaki kwenye mazishi na kwa bahati mbaya gari walilokuwa wanasafiria
lilichomoka tairi la mbele na kusababisha ajali hiyo iliyopoteza maisha
ya Idirsa pamoja na ngugu yake mwingine wa kike.
Hussein Ngulungu
amesema bado wanashughulikia kupata mwili wa marehemu na mazishi
yanategemewa kufanyika kesho mjini Morogoro mjini.
No comments:
Post a Comment