Pages

Monday, August 26, 2013

Pingamizi mwisho leo

UPOKEAJI wa pingamizi za wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na TPL Board unatarajiwa kufungwa leo mara baada ya pingamizi kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu TFF, Angetile Osiah.


Kamati ya Uchaguzi ya TFF, ilitangaza mchakato huo kuanzia Agosti 24 hadi leo saa 10:00 jioni kwa waweka pingamizi kuwasilisha pingamizi zao.

Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi huo, waweka pingamizi wote wanatakiwa kuzingatia matakwa ya ibara ya 11(3) ya kanuni za uchaguzi katika uwekaji pingamizi zao.

Mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Kamati ya Uchaguzi kesho inatarajiwa kukutana na walioweka pamoja na waliowekewa pingamizi ili kutoa utetezi wao juu ya pingamizi husika mbele ya kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Hamidu Mbwezeleni.

Baada ya kusikiliza pande hizo mbili, Kamati ya Uchaguzi itakuwa na fursa ya kupitia pingamizi husika ili kuendelea kwa zoezi hilo.

Wakati Uchaguzi Mkuu wa TFF ukipangwa kufanyika Oktoba 27, ule wa Bodi ya Ligi utafanyika Oktoba 18, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment