Pages

Monday, August 26, 2013

Yanga, Ashanti zaingiza mil. 102/-

MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Ashanti United iliyopigwa juzi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, imeingiza sh 102,856,000.
 
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kiasi hicho kimepatikana baada ya watazamaji 17,744 kukata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba moja ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa mabingwa watetezi Yanga kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-1.

Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 24,400,102.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 15,689,898.31.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 12,406,831.75, tiketi sh. 4,453,890, gharama za mechi sh. 7,444,099.05, Kamati ya Ligi sh. 7,444,099.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,722,049.53 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,894,927.41.

No comments:

Post a Comment