Pages

Tuesday, August 20, 2013

Temeke yaelemewa na watu

ONGEZEKO la idadi ya watu katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam kutoka katikati ya jiji na mikoani kunaisababishia manispaa hiyo mzigo wa kutoa huduma.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa manispaa hiyo, Joyce Msumba, alisema changamoto hiyo inahitaji rasilimali fedha ili kutoa huduma za jamii.

Alisema majukumu ya Serikali za Mitaa ni kutoa huduma kwa wananchi wake, bado kuna tatizo la wadau kushiriki katika ulipaji kodi, ushuru na ada mbalimbali katika halmashauri hiyo.

Changamoto nyingine inayoikabili halmashauri hiyo ni ongezeko la uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na utupaji ovyo wa takataka.

Nyingine ni ucheleweshwaji wa ruzuku kutoka Serikali Kuu, ujenzi holela wa makazi, uchache wa watendaji na vitendea kazi.

Katika hatua nyingine, alisema halmashauri hiyo imekusanya sh bilioni 25.1 katika mwaka wa fedha 2012/2013 kutoka sh bilioni 3.8 mwaka 2005/2006.
Msumba alisema fedha hizo zimetokana na vyanzo mbalimbali vya mapato yanayoizunguka halmashauri hiyo.

No comments:

Post a Comment