Pages

Monday, September 9, 2013

AGPAHI kumpa tuzo mwanamke anayeishi na mume mwenye virusi vya ukimwi (VVI).

SHIRIKA la Afya Linalopiga Vita Ukimwi na Utoaji wa Huduma za Kujikinga, Matunzo na Tiba kwa Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (Agpahi) limeahidi kumpa tuzo ya kuwa balozi mwanamke anayeishi na mume mwenye virusi vya ukimwi (VVI).

Mwanamke huyo ambaye hakupenda jina lake lichapishwe gazetini ni mke wa Mashauri Charles, mkazi wa Bukombe, Shinyanga ambaye makala yake ilitoka katika gazeti hili Septemba 5 mwaka huu.

Agpahi inafanya shughuli zake kwenye wilaya zote za mkoa wa Shinyanga ambapo hutumia dola milioni 1.4 za Marekani kwa mwaka kwa ajili ya kila halmashauri zenye kliniki za tiba na matunzo (CTC).

Akizungumza jana kwa njia ya simu, mkurugenzi wa shirika hilo, Laurean Bwanakunu, alisema ili kuwatia moyo na kuhamasisha mapambano dhidi ya VVU na ukimwi huwatumia wagonjwa waliopata ushauri wa kitaalamu kuwa walimu wa wagonjwa wengine.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, wagonjwa hao pia huwasaidia waganga wa CTC kutafuta namba au mafaili ya wagonjwa wenzao, kushuhudia watu na kuwahamasisha wapime afya zao.

“Tunatambua mchango wao ndiyo maana Agpahi huwapa posho kidogo kwa ajili ya shughuli hizo… huyo mama tutamfanya kuwa balozi wetu na tutamtumia pia akiwa tayari.
“…Wanaume wengi hawawezi hivyo wakishajua mke ameathirika wanamtimua lakini huyu mama kweli ni shujaa, tutamtumia kuwa mfano wa wanaopinga unyanyapaaji,” alisema Bwanakunu.

1 comment:

  1. Dada hata mm mme wangu ana virusi vya ukimwi na nimegundua baada ya mimi na yenye kwenda klinic sababu mm ni mjamzito kwaiyo tulienda klinic pamoja,kwa sasa nina mcimbwa ya miezi 9 ila naishi nae Kama kawaida ila natakiwa kuipata elimu ya kujikinga na mm nisiambukizwe maana siwezi kukutana nae kimwili naogopa

    ReplyDelete