Pages

Friday, September 27, 2013

Miss Universe Tanzania kujulikana leo

SWALI la nani atatwaa taji la Miss Universe Tanzania 2013, linatarajiwa kupata jibu leo wakati warembo 15 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania watakapochuana kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, mkabala na IFM jijini Dar es Salaam kuanzia saa moja kamili usiku.

Warembo hao mbali ya kuwania taji la Miss Universe Tanzania, ambalo kwa sasa linashikiliwa na Winfrida Dominique, pia watawania taji la Miss Earth Tanzania na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa.

Warembo hao kwa nyakati tofauti, wamekuwa wakitambiana huku kila mmoja akijigamba kutwaa taji hilo na kuiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia yaliyopangwa kufanyika jijini Moscow, Russia Novemba 9.
 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications inayoandaa mashindano hayo, Maria Sarungi, alisema kuwa kila kitu kimekamilika na warembo wamepania kufanya makubwa jukwaani, ambapo warembo wote wana ari ya juu na kila mmoja akiwa na shauku ya kutwaa taji hilo.

“Kwa upande wetu, kila kitu kiko tayari, warembo wamejiandaa vilivyo na tumeandaa shoo bora na fupi, hivyo mashabiki wa masuala ya urembo wanatakiwa kufika mapema ili kuona nani anatwaa taji na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi kimataifa,” alisema Maria.Warembo watakaochuana leo ni Aziza Victoria, Irene Nsiima, Betty Boniface, Kundi Mlingwa, Mariam Ngwangwa, Naomi Kisaka, Glady Msemo, Salsha Lukiko, Upendo Dickson, Vestina Mhagama, Angela Lutataza, Consolata Mosha, Clara Noor, Agnes Thobias, Dinah David na Clara Noor.

No comments:

Post a Comment