Pages

Sunday, September 8, 2013

MWILI WA MWANAMKE ALIYECHINJWA KIKATILI NA MUME WAKE WAAGWA

Mtoto wa marehemu aitwaye Baraka Simon akiaga mwili wa mama yake kwa simanzi.
Irene Kiwia akiaga mwili wa mfanyakazi wake.

     Ndugu na marafiki wakiaga mwili wa marehemu Yusta.
  Ilikuwa ni simanzi na majonzi.
MAITI ya mwanamke aliyeripotiwa kuchinjwa kikatili na mwanaume aliyesadikika kuwa ni mume wake, Yusta Ernest (28), ameagwa kwa majonzi makubwa kabla ya mwili wake kusafirishwa kwenda mkoani kwa mazishi.
 
Tukio hilo la kuagwa lilifanyika mapema leo hii katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar, na kuibua upya majonzi makubwa kwa ndugu na marafiki wa marehemu ambao wengi walionyesha wazi hisia zao kuwa wameumizwa na kifo cha kipenzi chao.
 
Akiongea kwa majonzi msemaji wa familia hiyo, Nelson Mgerwa alisema kuwa familia imeumizwa sana na kifo cha ndugu yao mpendwa ambaye ameondoka akiwa na umri mdogo.
 
Mwili wa marehemu umesafirishwa leo kuelekea Mpwapwa mkoani Dodoma, ambapo taratibu zote za mazishi zitafanyika katika kijiji cha Nzasa mkoani humo.
(Picha: Chande Abdallah / GPL)

No comments:

Post a Comment