Pages

Sunday, September 15, 2013

SERENGETI FIESTA KAMATA FURSA YAWAFIKIA VILIVYO WAKAZI WA MOROGORO

Msanii wa Hip hop, Nick wa Pili akiwapanua mawazo wakazi wa Morogoro na kuwapa mbinu zaidi za kutumia fursa zilizopo mkoani hapo.
Wakazi wa Morogoro waliohudhuria ukumbini hapo wakifuatilia kwa makini semina ya fursa.
Meneja Ujasiriamali wa Zantel, Haidar Chamshama, akiwaonyesha wakazi wa Morogoro namna ya kutumia fursa ya kubana matumizi kwa upande wa utumiaji wa simu za mkononi na kujua faida za simu zaidi katika kujikwamua kimaisha.
Mkuu wa Utafiti wa Maxcom Africa, Ahmed S Lussasi, akiwafafnulia wakazi wa Morogoro namna wanavyoweza kufaidika na bidhaa za Maxcom katika kujikwamua kimaisha.

Mtangazaji wa Kipindi cha Sport Extra cha Clouds FM, Shaffih Dauda akionyesha namna ya kutumia  fursa kwa upande wa michezo.
Mbunifu wa Mavazi wa Morogoro, Diana Magesa (kushoto), akizungumzia fursa ya mambo ya ubunifu, huku akionyesha mavazi yake kwa kumvisha Mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM,  Jelard Hando, ambaye alikuwa mshereheshaji wa semina hiyo.  
Mtalaam wa mambo ya Kilimo, Yona Joram, akiwafafanulia namna ya kutumia fursa kwenye upande wa kilimo.
Mwakilishi wa NSSF kutoka Makao Makuu, Salim Khalfani akizungumzia namna ya kutumia fursa zinazotokana na mafao ya NSSF kwa wakazi wa Morogoro leo ndani ya ukumbi wa Midland Hoteli mjini Morogoro.
Ruge akihitimisha Semina hiyo kwa kukaribisha maswali kutokana na mafunzo waliyoyapata wakazi wa Morogoro waliohudhuria kwenye semina ya Kamata Fursa Twenzetu mapema leo.
Baadhi ya wakazi waliokuwa ndani ya ukumbi huo wakiwa wamesimama baada ya kuombwa kuimba wimbo wa Tanzania na Mrisho Mpoto kabla ya kuanza kuonyesha fursa kupitia sanaa yake ya muziki.
Msanii wa kughani mashairi, Mrisho Mpoto akiwaimbisha wimbo wa Tanzania wakazi wa Morogoro muda mfupi kabla ya kuanza kutoa njia za kutumia fursa kupitia sanaa ya muziki.
SEMINA ya Kamata Fursa Twenzetu inayotolewa na timu ya Serengeti Fiesta 2013, kila mkoa inapotoa burudani, leo imeendelea tena kujenga na kupanua mawazo ya wakazi wa Morogoro katika mpango wa kuwawezesha kujua namna ya kutumia fursa zilizopo mkoani hapo katika kujikwamua kwenye maisha yao.

Semina hiyo ilifanyika mapema leo katika Ukumbi uliopo katika Hoteli ya Midland mjini Morogoro, ambapo baadhi ya wataalam kutoka sehemu mbalimbali walipata muda wa kuzungumza na wakazi hao na kuwajenga kwa kuwaonyesha njia mbalimbali za kujikwamua kimaisha.
(HABARI/PICHA:MUSA MATEJA/GPL, MOROGORO)

No comments:

Post a Comment