Pages

Sunday, September 8, 2013

Sofia Simba amzidi kete Anna Kilango

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sofia Simba, ameizidi kete kambi ya mpinzani wake, Mama Anna Kilango Malecela.

Sofia Simba ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ameizidi kete kambi ya Mama Kilango ambao waligomea uteuzi wa manaibu makatibu wakuu Bara na Visiwani, uliofanywa na Simba.

Habari ambazo Tanzania Daima Jumapili imezipata, zilisema kuwa baada ya kugomewa na kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Taifa ya Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) na kusababisha kikao kuvunjika, Waziri Simba sasa amefanikiwa kupitisha majina hayo na wateule hao sasa wameanza kazi.

Habari zinasema kuwa wajumbe wa kikao hicho ambao baadhi wanadaiwa kuwa ni wafuasi wa Mama Kilango waliopambana kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo taifa, waligomea uteuzi wa majina hayo kwa madai kuwa hawana sifa.

“Baada ya kugomewa, mwenyekiti aliwazidi kete kwa kwenda kwa rais na kumueleza sababu za uteuzi wa majina hayo na sasa watendaji wao wako ofisini,” kilisema chanzo chetu cha habari.

Wakati wa uchaguzi wa UWT, Waziri Simba ambaye alikuwa akitetea nafasi hiyo, alichuana vikali na Mama Kilango huku kila kambi ikidai kuchezewa rafu.

Katika kikao hicho kilichofanyika mwezi uliopita kwenye Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Dare es Salaam na kuvunjika, Mama Simba aliwasilisha jina la Salama Aboud Talib kutoka Zanzibar na Ever Kiwele wa Bara.

Vurugu kubwa zimetokea katika kikao cha utezi wa majina ya viongozi hao na kusababisha kuvunjika baada ya wajumbe kupinga uteuzi huo kwa madai kuwa hawana sifa.

Chanzo cha kuvunjika kwa kikao hicho ni vuta ni kuvute ya  nani ateuliwe kushika wadhifa wa Naibu Katibu Bara na Zanzibar.Chanzo Tanzania Daima.

No comments:

Post a Comment