Pages

Sunday, September 8, 2013

MAPOKEZI YA MBIO ZA MWENGE WILAYA YA TEMEKE 2013


Askari wakiupitisha Mwenge kwa ukakamavu kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bi Sofia Mgema.

Mbio za mwenge zilipiga kambi katika wilaya ya Temeke katika viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar hapo jana Septemba 08, ambapo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick (hayupo pichani)na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bi. Sofia Mgema walihudhuria mapokezi hayo.
Pia viongozi mbalimbali wa serikali, watumishi wa umma na wananchi kutoka sehemu tofauti  hapa jijini Dar waliokuwepo kwa pamoja waliupokea Mwenge huo na kushiriki michezo iliyoandaliwa kwa niaba ya kiongozi wa mbio za  Mwenge kwa mwaka huu, Juma Ali Simwai. Kauli mbiu ikiwa ni: “Watanzania ni wamoja tusigawanywe kwa misingi ya tofauti zetu za dini, itikadi, rangi na rasilimali.”
Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi za wilaya ya Temeke, wakionesha walichokiandaa.
Risala ikisomwa.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke akikabidhi Mwenge kwa Kiongozio wa Mbio za Mwenge, Juma Ali SimwaiJuma Ali Simwai (kushoto) akiwa ameketi sehemu aliyoandaliwa , kushoto ni wenyeji wake.Mkuu wa Wilaya ya Temeke akikabidhi Risala kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge
Juma Ali Simwai akitoa shukrani zake kwa Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sofia Mgema mara baada ya kukabidhiwa Risala.
(PICHA NA CHANDE ABDALLAH NA DENIS MTIMA/ GPL)

No comments:

Post a Comment