Pages

Friday, September 27, 2013

Soko la Kariakoo laelemewa na wateja kutokana na idadi kubwa ya watu 62,000 wanaoingia.

SOKO la Kariakoo jijini Dar es Salaam limeelemewa na wateja kutokana na idadi kubwa ya watu 62,000 wanaoingia na kutoka kila siku kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali.

Meneja Mkuu wa soko hilo, Florence Seiya, alibainisha hayo alipozungumza  ofisini kwake jana na kusema kwa siku soko hilo linahudumia watu 62,000.

Alisema mbali na kuelemewa na wateja, soko hilo linahitaji ukarabati utakaogharimu sh bilioni moja.

Alisema soko hilo lililojengwa miaka 39 iliyopita lina wafanyabiashara halali 1,558, mbali na wale wanaouza biashara za mkononi wanaojulikana kama ‘wamachinga’.

“Wafanyabiashara waliomo shimoni ni 600, walioko nje soko dogo ni 190, walioko ndani soko dogo ni 289, soko kubwa ni 189 waliobaki ni Mtaa wa Swahili eneo la soko,” alisema Seiya.

Seiya alisema kadiri siku zinavyokwenda nafasi inazidi kuwa ndogo, baada ya Shirika la Masoko Kariakoo kushindwa kujenga soko jingine la ghorofa la kisasa litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 4,000 kwa wakati mmoja.

Pia alisema kumekuwapo na ufinyu wa barabara za kuingilia sokoni hapo kutokana na magari mengi yanayoegeshwa katika soko hilo, mikokoteni, pikipiki na wale wafanyabiashara wanaofanya biashara zao kwenye barabara za lami.

No comments:

Post a Comment