Pages

Tuesday, October 1, 2013

Bomoa bomoa yatikisa Dodoma.

KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), Paskasi Muragili, amesema kuwa mpango wa kuwavunjia wananchi nyumba zilizojengwa katika maeneo yasiyopimwa uko pale pale.

Muragili alitangaza msimamo huo jana alipokuwa akizungumza na gazeti hili, akijibu malalamiko ya wakazi wa maeneo ya Kikuyu Kusini, Mkalama, Imagi, Miganga, Chinyika na Kata ya Mkonze, wanaopingana na CDA kwa kutaka kuwavunjia nyumba zao.

Kaimu mkurugenzi huyo alisema kama kweli mji wa Dodoma unatakiwa uwe jiji,   lazima ujengwe kwa ramani iliyopo ambayo imeboreshwa na si kuruhusu ujenzi holela.

Wananchi wa maeneo hayo waliilalamikia CDA kwa nadai kuwa imekuwa mwiba kwa wakazi wa Dodoma.

Ili kuonesha kukerwa na msimamo wa CDA, wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Kikuyu Kusini walirudisha kadi za chama hicho mbele ya diwani wao  kwa madai kuwa chama hicho hakiwajali wanyonge.

Tukio la kurudisha kadi za CCM lilitokea hivi karibuni katika mkutano wa hadhara ambao uliitishwa na wananchi kwa lengo la kujadili hatua ya CDA kutaka kubomoa nyumba zao.
Wananchi hao kwa nyakati tofauti katika mkutano huo, walidai kuwa wamechoshwa na CCM kwani inawakumbatia matajiri na kuwatelekeza wanyonge.
 
Hatua hiyo ya wananchi wa Kata ya Kikuyu, imetokana na barua ya CDA kuwaandikia wananchi wa eneo hilo kusisitiza kwamba mpango wa kubomoa nyumba zao upo pale pale

No comments:

Post a Comment