Pages

Saturday, October 19, 2013

Kortini kwa kumuua mkewe

MKAZI wa Chiringe wilayani Bunda mkoani Mara, Makeremo Mangasini  (33), amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Bunda, akidaiwa kumuua mkewe, Rehema Makelemo.

Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya hiyo Safina Simfukwe, ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Masudi Mohamed kuwa mnamo Oktoba 5 mwaka huu, majira ya saa kumi jioni, huko katika mtaa wa Chiringe, mshtakiwa alimpiga mkewe Rehema Makelemo kwa mateke na fimbo sehemu mbalimbali za nwili na kusababisha kifo chake.

Mwendesha mashtaka huyo aliiambia  mahakama kuwa siku ya tukio mshtakiwa baada ya kumpiga mkewe alipelekekwa na majirani katika hospitali ya DDH Bunda na muda mfupi baadaye alifariki akiwa anapatiwa matibabu.

Masudi alifafanua kuwa chanzo cha ugomvi wao ni wivu wa kimapenzi ambapo mume alikuwa akimtuhumu mkewe kwamba alikuwa akitoka nje ya ndoa yao.
Hata hivyo mshtakiwa huyo hakutakiwa kujibu lolote baada ya kusomewa shtaka lake kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria wa kusikiliza kesi hiyo.
Kesi hiyo itatajwa tena Novemba mosi wakati mtuhumiwa amerejeshwa rumande

No comments:

Post a Comment