MHE. MEMBE AZUNGUMZA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CUBA
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb.) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe. Bibi Ana
Teresita Gonzalez Fraga (kushoto) kuhusu masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba alipofika Wizarani kwa ziara yake
ya kikazi hapa nchini.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano, Bibi Dora Msechu akifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Membe
na Mhe.Fraga (hawapo pichani). Wengine ni Bw. Greyson Ishengoma
(katikati), Afisa Mambo ya Nje na Bw. Thobias Makoba, Msaidizi wa Waziri
Membe
Mkutano ukiendelea. Mwenye suti nyeusi ni Balozi wa Cuba hapa nchini, Mhe. Jorge Luis Lopes Tormo.
Balozi Msechu akiagana na Mhe. Fraga. Picha na Reginald Philip Kisaka.
No comments:
Post a Comment