Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.
RAIS Jakaya
Kikwete amekubali kuwavua vyeo vyao Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi
Vuai Nahodha, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David Mathayo
na Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki aliyekuwa tayari
ametangaza bungeni kujiuzulu. Taarifa hiyo imetolewa na Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda, bungeni baada ya kueleza kuwa ameongea na Rais na
kukubali kuwavua nyadhifa zao kutokana na ripoti ya Operesheni Tokomeza
iliyosomwa leo bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Mazingira, James Lembeli.
No comments:
Post a Comment