Pages

Monday, January 27, 2014

WANAFUNZI 1725 WASHINDWA KURIPOTI SHULENI WILAYA YA KILOLO

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo,Mh.Gerald Guninita akifungua kikao cha DCC katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya,Kushoto ni Mkurugenzi Ruukia Muwango na Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri  ya Wilaya,kikao kilichofanyika mwisho mwa wiki katika ukumbi wa halmashauri hiyo.
Mkurugenzi wa wilaya ya Kilolo Rukia Muwango akisoma taarifa ya wilaya hiyo mbele ya wajumbe wa kamati ya wilaya katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa wilaya mwishoni mwa wiki.
WANAFUNZI 1725  WASHINDWA KURIPOTI SHULENI WILAYA YA KILOLO
JUMLA ya wanafunzi 1725 waliotakiwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika shule mbalimbali zilizoko katika Wilaya ya Kilolo wameshindwa kuripoti kutokana na sababu mbalimbali.
 
Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashauri hiyo, Rukia Muwango  alisema wanafunzi wasioripoti kati ya hao wavulana walikuwa 788 na wasichana 937 sawa na asilimia 56.1

Muwango alisema wanafunzi waliochaguliwa kwa halmashauri ya wilaya ya Kilolo ni wanafunzi 3101 wavulana 1442, wasichana 1658 kati ya hao wavulana 10 na wasichana 10 wamechaguliwa katika shule za bweni.
Alisema wanafunzi waliopangwa kwenda katika shule za ufundi walikuwa wavulana 6 na hakuna msichana aliyechaguliwa na wanafunzi 3074 walipangwa katika shule za serikali katika halmashauri ya wilaya ya Kilolo.

Aliongeza kuwa wanafunzi walioripoti hadi Januari 23 mwaka huu walikuwa wanafunzi 1349 wakiwemo wavulana 638 na wasichana 711 sawa na asilimia 43.
Muwango alizitaja shule ambazo zina asilimia ndogo ya wanafunzi walioripoti shuleni kuwa ni shule ya Sekondari Mawambala (5.2%), Mlafu (14%), Lukosi (19.3%),Udekwa (21%) na Mtitu yenye asilimia 29 ya wanafunzi walioripoti.

Aliwataka walimu wa wakuu shule za sekondari wawasilishe majina ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 2014 waliojiunga katika shule zao ili halmashauri iweze kujua na kujiridhisha kuwa wanafunzi wote wapo shuleni na kutoa taarifa kwa wanafunzi wanaokwenda shule za zisizo za serikali kupata takwimu sahihi.
Alisema kuwa halmashauri imeandaa mikakati kwa wanafunzi wasioripoti kwa kuwaandikia barua waratibu wote kuwafatilia wanafunzi  hao na kuwahimiza kuhudhuria katika shule walizopangiwa.
 
Kwa upande wa ke Mkuu wa Wilaya hiyo Gerald Guninita amewataka watendaji wawasisitize wazazi kuwapeleka watoto shule bila kujali suala la ada na sare za shule.
Aliwataka watendaji kupeleka ripoti ndani ya siku 24 kwa wanafunzi wote ambao hawajaripoti shuleni hadi sasa katika ofisi ya wilaya na kuwachukulia hatua wazazi wakaidi.

“Haki ya mtoto kupata elimu ni muhimu sana na tusiache wazazi wanaowaficha watoto ndani hivyo wabanwe wazazi wao kwa kuwaficha kuna kitu nataka kuwaambia kumpeleka shule mtoto ni kumwongezea thamani mtoto na mzazi mwenye katika maisha yetu ya kila siku hivyo nawsisitiza sana watendaji wabaneni  sana wazazi wote wasiotaka kuwapeleka watoto wa kike shule” alisema Guninita.

No comments:

Post a Comment