Pages

Thursday, February 27, 2014

NAPE AUNGURUMA SHINYANGA AWAZOA WAWILI KUTOKA CHADEMA Thursday, February 27, 2014 Maoni: 0 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia matembezi ya mshikamano wakati yakiingia uwanjani kabla hajaanza kuhutubia wakazi wa Shinyanga mjini. Wakazi wa Shinyanga mjini wakiwa na Furaha ya kuwakaribisha wanachama wapya ambao walikuwa madiwani kwa kupitia Chadema ambao tarehe 25 walijiuzuru na tarehe 26 Februari 2014 kujiunga na CCM. Zakaria Martin Mfuko aliyekuwa Diwani wa Chadema Kata ya Masekelo akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo na kuwaambia wananchi hao ameamua kurudi CCM kutokana na ufisadi na ukiukwaji ya maadili ya Uongozi ndani ya Chadema. Sebastian Peter maarufu kama Obama aliyekuwa Diwani wa Chadema kata ya Ingokole akihutubia wananchi kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo mjini Shinyanga. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimsaidia kufunga vifungo vya shati Ndugu Sebastian Peter aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ingokole ambaye amerudisha Kadi yake ya Chadema na kupokelewa rasmi CCM kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo mjni Shinyanga. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia maelfu ya wakazi wa Shinyanga mjini na kuwaambia Huu ndio Mwanzo tu,aliwaambia CCM imejengwa kwa misingi imara hivyo itaendelea kuwepo kwa muda mrefu zaidi. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimpa ushauri Mbunge wa Shinyanga Mjini Ndugu Stephen Masele juu ya VETA mkoani hapo kutoa kozi zinazoendana na mahitaji ya Soko la Viwanda vya Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mahakama ya mwanzo Shinyanga mjini tarehe 26 Februari 2014. TAARIFA YA KUPOTEA KWA BIBI HUSNA NCHINI MALAYSIA . Thursday, February 27, 2014 Maoni: 0 Tunamtafuta Bibi Husna ambaye asili ya kimalaysia, aliolewa na Mtanzania Baba yake ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa ni Bw. Said Abdullah Belwal. Kwa taarifa Husna ni Muuguzi (Nurse) ila haifahamiki hospitali gani na mji gani. Mume wake ni Mwanajeshi na ndoa yao ilifungwa kijeshi. Tafadhali atapopata tangazo hili au yeyote mwenye taarifa zake awasiliane na namba hizi Mob: +60102987357 Tel: +60342517603 Kuala Lumpur, Malaysia Email: apoloniamwangosi@yahoo.com KINGWENDU AJA NA FAZA HAUSI Thursday, February 27, 2014 Maoni: 0 MSANII wa filamu nchini Athumani Lali 'Budege' baada ya kucheza filamu za watu sasa ameamua kuja na filamu zake mwenyewe na kuwawezesha wasanii wenzie kuwa na kipato kizuri baada ya kuamua kufungua kampuni yake binafsi inayokwenda kwa jina la AJM Entatainment ambayo ina husika na maswala ya filamu za kibongo Athumani Lali 'Budege' Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Lali amesema kuwa kwa sasa yupo katika atua za mwisho kwa ajili ya kutoa filamu mpya inayokwenda kwa jina la Faza Hausi ambayo imeshilikisha wasanii wakongwe ndani yake akiwemo Mohamed Nurdini 'Chekbudi' ,Esha Buheti, Rashidi Mwishehe 'Kingwendu' Muogo Mchungu . Filamu hiyo itakayo tolewa na Kampuni hiyo ya jijini Dar es salaam itakuwa moto wa kuotea mbali kwani si ya kukosa kabisa kwa mashabiki wa filamu nchini. filamu hiyo ya Faza Hausi itakuwa mtaani wakati wowote kuanzia sasa kwani takribani vitu vyote muhimu vimeshafanyika hivyo wadau wakae mkao wa kula kwani filamu hii si yakuikosa Ambapo itapatikana Tanzania nzima nikianzia Dar es salaam na mikoa yote filamu hiyo itawafikia WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WAFANYA ZIARA TBL JIJINI DAR


 Wahariri wakiwa katika picha ya pamoja a viongozi wa TBL wakati wa ziara hiyo.
 Wahariri wa Vyombo vya Habari wakitembelea eneo la upikaji bia wakati wa ziara yao iliyofanyika  kwenye Kiwanda cha Bia Tanzania cha Dar es Salaam
 Mtalaam wa Upishi Bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Benjamin Budigida akitoa maelezo ya jinsi bia inavyopikwa kwa kutumia njia ya kisasa ya kompyuta  wakati wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari walipotembelea Kiwanda cha Bia cha TBL Dar es Salaam.
 Meneja wa Usimamizi wa Ubora wa Bia wa TBL, Conchesta Ngaiza (kulia) akielezea jinsi wanavyodhiti ubora wa bia.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzsche (kushoto) akisalimiana na Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Nevile Meena wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo  vya habari katika Kiwanda cha Bia cha TBL Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa TBL, Kelvin O'Flaherty.

No comments:

Post a Comment