Pages

Monday, March 3, 2014

SHAMSA: MSIMSOGELEE MUME WANGU!

MWADADADA anayefanya poa Bongo Movies, Shamsa Ford amewataka wanawake wanaomfuatilia mumewe, Dickson waache mara moja.
Shamsa Ford.
Shamsa alisema, anakerwa sana na tabia ya wanawake wanaomfuata mumewe kwani hata wale wa ‘zilipendwa’ wameanza kujirudisha upya kitu ambacho hatakubaliana nacho.
“Hawa wanawake hawana adabu wala aibu, ninawatahadharisha tu, wakae  mbali na mume wangu kabla sijawaanika hadharani kwenye vyombo vya habari, kwanza hawawezi kufanikiwa, najiamini,” alisema Shamsa.

No comments:

Post a Comment