Pages

Saturday, April 26, 2014

UOZO MAHOSPITALINI: OFM YAIFUNGIA KAZI PALESTINA!

BADO hali ya huduma zinazotolewa na baadhi ya hospitali zetu nchini ni mbaya, utendaji mbovu na wagonjwa hawajaliwi hata pale inapotokea wamepelekwa wakiwa mahututi, Risasi Jumamosi linakufunulia.
Eneo la hospitali ya palestina.
Baada ya kuanika uozo wa hospitali kadhaa – za serikali na binafsi, sasa kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global Publishers, kilitinga katika Hospitali ya Wilaya ya Kinondoni, Palestina na kugundua udhaifu mkubwa wa huduma mbovu zitolewazo hospitalini hapo.
OFM wakiingia hospitalini hapo.

YALITANGULIA MALALAMIKO
Wananchi mbalimbali kwa nyakati tofauti walipiga simu kwa OFMna kueleza namna hospitali hiyo inavyotoa huduma mbaya hasa Mapokezi, wauguzi na madaktari wa kitengo chote cha wagonjwa wa nje, ‘Outpatient Department’ (OPD).
OFM wakiwa chumba cha daktari bila ya uwepo wa daktari.
OFM KAZINI
Aprili 23, mwaka huu saa 10:42 za alasiri, OFMwaliingia hospitalini hapo wakiwa tayari kwa kazi, ambapo mmoja wao alijifanya mgonjwa mahututi aliyehitaji huduma ya haraka.
Wakiwa chumba cha manesi huku manesi wakiwa hawapo ofisini.
Walipofika Mapokezi, pamoja na kuonekana mgonjwa kuwa na hali mbaya, wahudumu hawakumpa kipaumbele na kuendelea kuwahudumia wagonjwa wengine kwa foleni ambao hawakuonekana kuwa ‘serious’ sana.
Mgonjwa akiwa amelalala kwenye benchi kusubiri huduma.
Baada ya dakika 12 kupita bila msaada, mpelelezi mmoja wa OFMaliyejifanya ni mwanafunzi mwenzake na mgonjwa, alikwenda dirishani kuomba kuandikiwa kadi haraka ili aende kwa daktari, akapewa.
FOLENI NDEFU, HAKUNA DAKTARI
Mapaparazi wa OFMwakiwa na mgonjwa wao kwenye baiskeli ya wagonjwa, walifika kwenye foleni iliyokuwa na watu wengi wanaohitaji kuingia kwa daktari lakini hakuwepo ofisini kwake, zilipita dakika 14 ndipo akatokea.
Hata hivyo manesi waliokuwa wakirandaranda kwenye korido hawakutoa msaada wowote kwa wagonjwa waliokuwa wanamsubiri daktari.
MAIGIZO CHUMBANI KWA DAKTARI
Mgonjwa akionekana kuzidiwa sana (alipatia kweli kuigiza mgonjwa!) alimweleza daktari kuwa alikuwa akisumbuliwa na maumivu makali mwilini, viungo kufa ganzi na shida katika mfumo wa upumuaji.
Hata hivyo, mgonjwa huyo alimweleza daktari kuwa hali hiyo ilimpata ghafla akiwa na wenzake chuoni, haikuwahi kumtokea kabla.
Baada ya kumpima shinikizo la damu, mgonjwa huyo alionekana yupo katika hali ya kawaida, kipimo kilisoma 110/70 mmHg.
TIBABILAVIPIMO
Katika hali ya kushangaza daktari huyo, bila kumpima mgonjwa ili kuthibitisha anachoumwa, aliagiza kwanza achomwe haraka sindano mbili – Diclofenac (ya maumivu) na Hydrocortisone (ya kutuliza maumivu ya kifua).
Kwa msaada wa wenzake, mgonjwa huyo alipelekwa chumba cha sindano na kukubali kuchomwa sindano ya Declofenac kwa vile walijua ni ya maumivu tu lakini wakagoma mgonjwa wao asichomwe ile nyingine mpaka watakapopewa maelezo inatibu ugonjwa gani.
MAABARA
Baada ya kuchomwa sindano hizo alitakiwa kuelekea maabara kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa vipimo mbalimbali ikiwemo cha malaria ambacho kitaalamu kiliandikwa RDT (Rapid Diagnostic Test for Malaria) na RPG.
Mapaparazi wetu walishuhudia wagonjwa wengi wakiwa kwenye foleni huku wengine wakiwa na hali mbaya kwenye baiskeli za wagonjwa wakisubiri huduma.
Paparazi wetu alilazimika kujilaza kwenye fomu katika foleni na kusubiri hapo kwa takribani nusu saa ndipo alipochukuliwa vipimo na kuletewa majibu baadaye yaliyoonyesha hakuwa na ugonjwa wowote.
Kwa kuwa kazi ilikuwa imeshakamilika, mapaparazi wetu hawakuona sababu ya kurudi kwa daktari, walitokomea zao mitaani na mgonjwa feki wao ambaye alionekana kuanza kupata nafuu.
MGANGA MKUU KIKAANGONI
Alhamisi, Aprili 24, mwaka huu, mishale ya saa 6:30 mchana, mmoja wa makachero wa OFMalifika hospitalini hapo na kuonana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina, Dk. Benedict Luoga ili azungumzie tuhuma hizo.
Baada ya kusikiliza madai hayo, Dk. Luoga alikataa kuzungumza kwa maelezo kuwa yeye siyo msemaji, badala yake akamwelekeza mwandishi huyo kwenda kwa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk. Gunini Kamba aliyedai ndiye msemaji.

No comments:

Post a Comment