KATIKA
kuhakikisha wanafanya vyema kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara pamoja na
michuano ya kimataifa, Klabu ya Azam inatarajia kuweka kambi nchini
Hispania ikiwa ni sehemu ya maandalizi.
Azam ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu, wanatarajia kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo kilisema kuwa, klabu
hiyo imepanga kuweka kambi yake nchini humo kwa lengo la kulinda heshima
mara baada ya kutwaa ubingwa wa ligi.
Aidha, kilisema kocha wa timu
hiyo, Mcameroon, Joseph Omog, anatarajia kurejea kati ya Juni 13, mwaka
huu huku kambi ikianza Juni 16.
“Kambi imepangwa kuwa Hispania, lengo likiwa ni kuwapa nafasi
wachezaji kujifunza vitu vingi kama ambavyo inajulikana nchi hiyo kwa
soka la uhakika, pia mwalimu anaweza kutua Dar kati ya Juni 13,”
kilisema chanzo hicho.
Championi lilimtafuta katibu wa timu hiyo, Idrissa Nassor na kuhoji
kuhusiana na ishu hiyo ambapo alisema: “Klabu imempa jukumu kocha Omog
aamue yeye kambi anataka iwekwe wapi kwa kuwa anajua wapi patamfaa.”
No comments:
Post a Comment