Pages

Friday, June 6, 2014

Mwenyekiti Tawi la Yanga afariki dunia

Na Daudi Juliani, Morogoro
MWENYEKITI wa Tawi la Yanga Safi lililopo Mji Mpya mkoani Morogoro, Injinia Khamisi Katoto, amefariki dunia kwa ajali ya gari.
Katibu wa tawi hilo, Khamisi Mkingiye ameliambia Championi Ijumaa kuwa, ajali hiyo ilitokea eneo la Kihonda Maghorofani, Manispaa ya Morogoro na kusababisha kifo cha mwenyekiti huyo.
Mkingiye alisema kifo hicho ni pigo kubwa kwa tawi hilo na kwa tasnia ya mchezo Moro kwa kuwa marehemu alikuwa mstari wa mbele kulitafutia maendeleo tawi hilo.

No comments:

Post a Comment