Pages

Friday, June 6, 2014

Mbeya City wakatazwa kusajili

KOCHA wa zamani wa timu ya taifa, Taifa Stars, Sylvester Marsh ameyatazama mafanikio ya timu ya Mbeya City ya msimu uliopita na akamshauri kocha mkuu wa timu hiyo, Juma Mwambusi kuwa, kama anataka kufaidika zaidi msimu ujao hatakiwi kusajili wachezaji wapya.
Marsh ambaye alikuwa kocha msaidizi wa Stars chini ya utawala wa Kocha Mkuu, Mdenishi, Jan Poulsen kabla ya kukabidhiwa mikoba kocha wa sasa, Mdachi Mart Nooij, ameifafanua kauli yake hiyo juu ya timu hiyo iliyomaliza Ligi Kuu Bara msimu uliopita ikiwa nafasi ya tatu.
Marsh amesema timu hiyo imeenea kila idara na wala haihitaji marekebisho ya wachezaji wa nje kwa ajili ya kuiboresha, badala yake ni kuwaongezea morali wachezaji waliopo.
“Unajua wale wachezaji hawana majina ila wana morali ya juu, wanapaswa kudumisha umoja wao, lakini ukiwaletea wapya kipindi hiki ambacho timu ipo kwenye fomu, watakuja na tabia zao tofauti na kuambukiza vitu vipya,” alisema Marsh.

No comments:

Post a Comment