Pages

MLAPA NG’OSHA: KALALE PEMA (OFFICIAL VIDEO)

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva anayekuja kwa kasi, Gabriel Samalu Ng’osha ‘Mlapa Ng’osha' ameachia video yake mpya inayokwenda kwa jina la 'Kalale Pema' aliyoelezea maisha ya mateso anayopata mama mjamzito.
Mojawapo ya picha katika video hiyo.
Video hiyo imetengenezwa chini ya prodyuza Melkiadi Oreje 'OJ' wakati audio ikifanywa na Lebo ya Audio Visual ya nchini Kenya chini ya maprodyuza Haptune & Douncher.

JIHAN DIMACHK NDIYE REDD'S MISS TANZANIA TOP MODEL 2014



Mshindi wa taji la Redd’s Miss Tanzania Top Model 2014, Jihan Dimachk (katikati) akipozi kwa picha na mshindi wa pili Doreen Robert (wapili kulia), mshindi wa tatu Evelyn Baasa ambaye pia ni Miss Tanzania Photogenic 2014 (wapili kushoto), mshindi wa nne, Lilian Timothy (kulia) na Mshindo wa tano Nasreen Abdul, mara baada ya kushinda taji hilo jana ambapo Jihan amekuwa mrembo wa pili kuingia katika nusu fainali za Miss Tanania 2014 baada ya Miss Photogenic. Shindano la Miss Tanzania Top Mode lilifanyika katika ukumbi wa Triple A jijini Arusha na kuwashirikisha warembo 30.

MKUTANO WA JUMUIYA YA WATANZANIA SWEDEN NA KUMKARIBISHA BALOZI DORAH MSECHU

 Mama Dora Msechu Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchi za kinordic na Baltic alipokelewa kwa shangwe.
 Muziki hadi lyamba

Taarifa Za Msanii Mwingine Wa Bongo Fleva Kufariki Dunia

side
Taarifa zilizonifikia muda huu ni kuwa msanii chipukizi kwenye muziki wa Bongo Fleva Side Boy amefariki dunia. Kwa mujibu wa mdogo wake Ally Khamis, anasema Kaka yao marehemu Said Salum Hemedy amefia Lindi kwenye hospitali ya Nyangao, Alikuwa akisumbuliwa na TB Ya mifupa.
Hii ndio video yake Hujafa hujaumbika,alifanya na Besti Naso.

JWTZ MILIONEA ALIVYOUAWA KWA RISASI

CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
NI taharuki iliyojaa majonzi na simanzi kufuatia Jeshi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’ Kikosi cha CMTU jijini Dar kuondokewa na mpiganaji wake, Sajenti Yohana  Lugendo Gweso (40) ambaye alikuwa milionea aliyepigwa risasi sita mwilini na kufariki dunia papo hapo.
Mwili wa marehemu Sajenti Yohana Lugendo Gweso (40) wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’ Kikosi cha CMTU ukiwa kwenye jeneza.
Tukio hilo la kusikitisha, lilijiri saa 1:45 usiku wa Septemba 22, mwaka huu, Ukonga Babana ndani ya baa maarufu ijulikanayo kwa jina la Super Karatu.
UWAZI HATUA KWA HATUA
Kufuatia tukio hilo, Uwazi kama kawaida yake lilifuatilia kwa kina ili kubaini yaliyofichika nyuma ya pazia kama siyo sirini!

PAKA AFUNGWA HIRIZI MTINI...ASHUTUA WANANCHI MTAANI WAHOFIA MAISHA YAO

Stori: Dustan Shekidele, MOROGORO KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, paka mwenye hirizi kubwa shingoni akiwa hai alikutwa amepigiliwa misumari juu ya mti uliopo jirani na Msikiti wa kwa Mtawara uliopo Kata ya Mwembesongo mkoani hapa.
Paka mwenye hirizi kubwa shingoni akiwa amepigiliwa misumari juu ya mti uliopo jirani na Msikiti wa kwa Mtawara uliopo Kata ya Mwembesongo, Morogoro.
Tukio hilo lililokusanya umati mkubwa wakiwemo waumini wa msikiti huo lilitokea alfajiri ya Alhamisi iliyopita ambapo baadhi ya waumini wa msikiti huo walikuwa wamefika msikitini kwa Swala ya Alfajiri.

Monday, September 29, 2014

Hizi ndio gari mbili alizopewa Wema Sepetu kama zawadi ya Birthday


Miss Tanzania 2006 ambae bado analinda jina lake lisipotee midomoni mwa watu Wema Abraham Sepetu, ameshangazwa na watu wake wa karibu kwa zawadi alizopo
Wema alipokea gari mbili ambapo moja alipewa na Mpenzi wake Chibu Dangote "Diamond Platnumz" aina ya Nissan Murano ipo kwenye hapo chini pamoja na BMW ambayo hii wengi hawakujua imetoka kwa nani lakini baadae ukweli umetambulika kwamba imetoka kwa Kaka Manager Martin Kadinda. Martin amemkabidhi Wema gari hilo pamoja na kadi ya Gari ikiwa imeandikwa jina lake.
 Hii ndio Nissan Murano aliyopewa na Diamond
Martin Kadinda akimuonesha Wema Sepetu kadi ya gari
Wema Sepetu baada ya kutoka nje na kuona gari hiyo
PICHA NA MTANDAO

DIAMOND AMZAWADIA WEMA MURANO


 

Gari aina ya Nissani Murano alilozawadiwa Wema Sepetu na mpenzi wake Diamond Platnumz.
STAA wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amemzawadia gari aina ya Nissan Muran mpenzi wake Wema Sepetu katika bethidei yake jana.
Kupitia ukaunti yake ya Instagram, Diamond ameandika hivi:

RAY C SASA ATAKA KUOLEWA NA MZEE!

 
Utu uzima dawa! Staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amefunguka kuwa kwa sasa hana mpenzi wala hajapata mtu wa kumuoa ila anataka kuolewa na mzee atakayeweza kumlea.
Staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Akizugumza na wanahabari wetu kwenye mgahawa wake wa Ray C uliopo Mwananyamala, Dar, mwanadada huyo alisema yeye kama mwanamke anatamani kuolewa na kupata mtoto si na ‘serengeti boy’ bali mzee.
Aliendelea kutiririka kwamba akikosa wa kumuoa atatafuta mwanaume atamlipa kwa ajili ya kuzaa naye tu lakini ni pale atakapokuwa anaweza kulea  mwenyewe.
Ray C aliongeza kuwa, kwa sasa anatafuta wadhamini kwa ajili ya kuendesha taasisi yake ya Ray C Foundation kwani amefanikiwa kuwasaidia watu wengi kupata kazi na kuachana na dawa za kulevya.
 Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya/GPL

WEMA AWACHARUKIA WASANII WENYE MAJUNGU

MADAMUUU! Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amecharuka na kudai anachukizwa kwa kiasi kikubwa na wasanii ambao wanapenda kumfanyia majungu kutokana na chuki zao binafsi.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Madam alisema anajua wapo wengi wanaomchukia kutokana na sababu zisizo za msingi kwa kudai kuwa anaringa na vyovyote vile wanavyojadili lakini hajali kwa kuwa hakuna ukweli wowote.
“Watu wenye majungu hawanisumbui kichwa kabisa nabaki nawatazama tu, sababu sina maringo wala majivuno kwa mtu yeyote, sasa cha ajabu wengine wanasema naringa, kwa staili hiyo hatutafika mbali maana wasanii wa nchi za wenzetu wana umoja hawana mambo ya aina hiyo,” alisema Wema.

KABURI LA RECHO LALOA MACHOZI!


 
Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
Roho inauma! Kwa mara nyingine, kaburi la aliyekuwa staa wa sinema za Kibongo, Rachel Leo Haule ‘Recho’ (pichani) limeloa machozi ya mastaa wakati wa kusimikwa msalaba baada ya kujengwa na kuonekana la kisasa, Ijumaa Wikienda lilikuwepo.
Mchungaji akiongoza ibada ya kubariki na kuutakasa msalaba utakaowekwa kwenye kaburi la marehemu Recho Haule.
Katika tukio hilo lililojiri wikiendi iliyopita, vilio vya mastaa vilianzia Kanisa la Anglikana lililopo Magomeni-Mwembe Chai, Dar ambapo ilifanyika ibada maalum kwa ajili ya kumuombea marehemu huyo na wengine waliotangulia mbele ya haki.

WEMA, DIAMOND WANADAIWA KUFANYIANA 'TIMINGI' YA KUMWAGANA!

Diamond..Mh! Upepo mbaya unaivumia kapo ya mafahari wawili Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambapo wanadaiwa kufanyiana ‘taimingi’ ya kumwagana, Ijumaa Wikienda linakupa ‘ubuyu’ kamili.
Staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu makini, wawili hao wamepotezeana kwa muda mrefu huku kila mmoja akifanya yake lakini kila mmoja anashindwa kujitoa mhanga na kusema hawapo pamoja akihofia kuonekana ndiye tatizo.
“Kifupi ni kwamba Wema na Diamond hawapo pamoja kwa kipindi kirefu, yawezekana wanawasiliana lakini si kwa mapenzi labda kwa mambo mengine. Diamond anazuga kama yuko kwenye shoo, hata akirudi Bongo hawana ukaribu na Wema kama ilivyokuwa zamani, anazuga kidogo kisha anaondoka tena.

ROSE NDAUKA MCHUMBA'KE WAACHANA!

Stori: Imelda Mtema Ooh…nooo! Wachumba wa muda mrefu, staa wa sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka na Malick Bandawe ambao maisha yao ya kimapenzi yamekuwa yakitawaliwa na msuguano wa chini kwa chini, hatimaye wameachana, Ijumaa Wikienda linakupa mkanda mzima.
Staa wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini na cha uhakika kimemwaga data kwamba wachumba hao ambao walivalishana pete kwa mbwembwe miaka mitatu iliyopita huku wakipika na kupakua lakini wamekuwa katika mzozo wa muda mrefu wa kifamilia, ambapo mara kadhaa wameripotiwa kuchapana wameachana.

Saturday, September 27, 2014

MASHINDANO YA VIPAJI VYA WANAWAKE (WOMEN TALENT SYSTEM) YALIVYOFANA KATIKA HOTELI YA JB BELMONT

 Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Azikiwe, Fabiola Massula (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Mshereheshaji wa shoo hiyo. Benki hiyo ni mmoja wa wadhamini wa shoo hiyo.
Mkurugenzi wa Women Talent System, Angels Howell (katikati) akizungumza jambo kuhusiana shoo hiyo (kulia kwake), Meneja kutoka Mmi Tanzania, Paolo Frattari.
Rais wa Shirikisho la Dunia la mchezo wa Karate (UPAM), Profesa  Martina Maurizio (kushoto), akipiga makofi kushiria kufuraishwa na jambo wakati wa mashindano ya vipaji vya wanawake (WOMEN TALENT SYSTEM) ilifanyika Septemba 25,2014 katika Hotel ya JB BELMONT jijini Dar es Salaam.

MAFUNZO YA MWEZI MMOJA YA OLIMPIKI MAALUMU TANZANIA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU WA AKILI YA FUNGWA RASMI

Walimu waliokuwa wakiendesha mafunzo kwa watoto hao wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Beatha Qambayot, Zilpa Masunga, Mtendaji Mkuu wa Olimpiki Maalumu Tanzania, Frank Macha na Alphonsia Mwairafu.
Walimu hao wakiwa wameshika mipira ya kufundishia. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Watoto wenye ulemavu wa akili wakiwa katika picha na  wazazi, pamoja na walimu wao baada ya kumaliza mafunzo  ya mwezi mmoja ya Olimpiki Maalumu Tanzania  yaliyofikia tamati wilayani Temeke Dar es Salaam leo.

MZIKI MNENE WA EFM WATIKISA BAGAMOYO

Mashabiki wa  kituo kipya cha EFM 93.7 Radio wakicheza Mziki mnene ndani ya Bagamoyo.
Mashabiki wakiendelea kupagawa na burudani.

FIESTA YAWAPAGAWISHA WAKAZI WA SONGEA

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Recho akifanya makamuzi kwenye Tama...Recho akiwajibika jukwaani hapoBaadhi ya mashabiki wapagawa na makamuzi ya mwanadada Recho

WEBSITE & BLOGS DESIGN CAL: 0755 451 999.

Tunatengeneza Website na Blogs Zenye Mvuto wa kuvutia na tunatoa training Muda wote 
Mawasiliano : 0755 451 999