Pages
▼
Wednesday, December 31, 2014
RAYUU AMUANIKA MWANDANI WAKE
Stori: Mayasa Mariwata
MSANII wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amezua gumzo baada ya picha zake zinazomuonesha akiwa chumbani na mwanaume kuenea mtandaoni, huku kijana huyo akionekana kujichora tatoo yenye jina la mwanadada huyo.

Kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja la Brown hakuweza kupatikana ili kuthibitisha uhusiano wake na mrembo huyo, lakini Rayuu alikiri kuwa ingawa picha iliyowekwa mtandaoni ilionyesha wakiwa kikazi zaidi, huyo ni mpenzi wake wa siku nyingi.

WELLU ANASA MIMBA TENA!
Stori: Waandishi Wetu
IMEVUJA! Msanii wa filamu Bongo, Wellu Sengo, ‘Matilda’, licha ya kuwa na mtoto mdogo ambaye hajafikisha hata mwaka, inadaiwa tayari amenasa ujauzito mwingine.Chanzo makini kinaeleza kuwa ujauzito huo ni wa mmoja wa wasanii wenye majina maarufu hapa nchini, ambao wamekuwa katika uhusiano kwa muda mrefu sasa.
DOKTA AONYA MIMBA YA AUNT!
TABIA za mitoko ya usiku matembezini, uvaaji viatu virefu na unywaji
pombe unaofanywa na wamama wajawazito, kama alivyo sasa muigizaji Aunt
Ezekiel, zimeelezewa kuwa si nzuri na zina uwezekano mkubwa wa
kusababisha madhara kwa mtoto anayetarajiwa kuzaliwa.
Akizungumza baada ya kuulizwa na gazeti hili juu ya mwenendo wa muigizaji Aunt Ezekiel ambaye mara kadhaa huonekana akiwa ‘viwanja’ usiku, daktari mtaalamu wa magonjwa ya kina mama na watoto, aliyejitambulisha kwa jina moja la Dokta Chale, alisema utokaji wa usiku na uvaaji wa viatu virefu unaweza kusababisha matatizo ya nyonga, shida wakati wa kujifungua, miguu kuuma na uvimbe kwenye vifundo vya miguu ‘enka’.

Tuesday, December 30, 2014
DIAMOND PLATNUMZ ATUA RWANDA KWA SHANGWE
Staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akiwa na mfanyabiashara mrembo na muimbaji wa Uganda, Zarinah Hassan 'Zari' au 'The Boss Lady' baada ya kuwasili Rwanda jana.
WAIMBA INJILI WANA NINI?
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
MENGI yameibuka kufuatia waimba Injili Bongo kukumbwa na kashfa mbalimbali zikiwemo ndoa zao kuvunjika, madai ya kuchepuka, kupata ujauzito nje ya ndoa na matumizi ya madawa ya kulevya, Uwazi limechimba na kuchimbua.
BADO JINAMIZI LA KUVUNJA NDOA LAWAANDAMAMENGI yameibuka kufuatia waimba Injili Bongo kukumbwa na kashfa mbalimbali zikiwemo ndoa zao kuvunjika, madai ya kuchepuka, kupata ujauzito nje ya ndoa na matumizi ya madawa ya kulevya, Uwazi limechimba na kuchimbua.
Mpaka sasa, waimba Injili wanawake wameshakumbwa na mikasa mbalimbali lakini mpya kabisa ni madai ya hivi karibuni kwamba, ndoa ya mwimbaji mwingine, Kabula George imesambaratika.
Kabula George mwaka 2012 alitamba na Albamu ya Nitang’ara Tu! Inadaiwa hayuko kwa mumewe baada ya ndoa yao kudumu kwa miaka nane!
JANET MREMA ANAUMWA
Huyu aliwahi kuripotiwa na Gazeti la Amani miezi miwili iliyopita kwamba, ndoa yake na mumewe, Jonas Mrema imesambaratika madai makubwa ni mume kutomwamini mkewe huyo na kudai alitoroshwa nyumbani na mchungaji mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) aliyejulikana kwa jina moja la Emmanuel.
Habari mpya ni kwamba kwa sasa hali yake ni tete, anaumwa lakini
wengi wanaamini ugonjwa wake unatokana na mawazo ya kuchanika kwa ndoa
yake.Tayari mwanaume huyo ameshafungua kesi Mahakama ya Kinondoni, Dar
akimlalamikia Mchungaji Emmanuel kumtoroshea mkewe. Anataka fidia ya
pesa ambazo mahakama itaamua kama itaona ni sahihi.Huyu aliwahi kuripotiwa na Gazeti la Amani miezi miwili iliyopita kwamba, ndoa yake na mumewe, Jonas Mrema imesambaratika madai makubwa ni mume kutomwamini mkewe huyo na kudai alitoroshwa nyumbani na mchungaji mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) aliyejulikana kwa jina moja la Emmanuel.
BAHATI BUKUKU
Huyu ni mwimba Injili mkongwe Bongo. Ndoa yake na Daniel Basila ilivunjika mwaka 2005, mume alimtuhumu Bahati kutoroshwa nyumbani na mzungu mmoja ambaye hakumtaja jina.
Baadaye Bahati alikanusha, akasema aliamua kuondoka nyumbani kwa Daniel kutokana na manyanyaso mengi. Alishindwa kuvumilia. Mpaka sasa, Bahati hayuko kwenye ndoa.
NEEMA MWAIPOPOHuyu ni mwimba Injili mkongwe Bongo. Ndoa yake na Daniel Basila ilivunjika mwaka 2005, mume alimtuhumu Bahati kutoroshwa nyumbani na mzungu mmoja ambaye hakumtaja jina.
Baadaye Bahati alikanusha, akasema aliamua kuondoka nyumbani kwa Daniel kutokana na manyanyaso mengi. Alishindwa kuvumilia. Mpaka sasa, Bahati hayuko kwenye ndoa.
Alipovuma sana na wimbo wa Sipati Picha alikuwa akijulikana kwa jina la Neema Mushi. Mumewe ndiye Mushi. Baadaye, ndoa yake ilivunjika, akarudia jina la ukoo wake, Mwaipopo. Akatoa albamu inaitwa Raha Jipe Mwenyewe.
BONDI, WASTARA PENZI LAO KIZUNGU-MKUTI
BAADA ya wiki iliyopita msanii wa filamu Bongo,
Wastara Juma kuripotiwa kwenye moja ya magazeti pendwa kuwa hana
uhusiano na mtu yeyote ndani ya Bongo Muvi na yupo mbioni kumuanika
mrithi wa Sajuki mengi yameendelea kuibuka.
Akizungumza na Uwazi, mpenzi wa Wastara anayetambulika kwa jina la Bondi Bin Salim alidai kuwa yupo kwenye mchakato wa mwisho wa kutoa mahari kwa ndugu wa msanii huyo kiasi cha shilingi milioni 5 pamoja na pete za dhahabu ili aweze kuwa na Wastara.
Alisema kuwa maamuzi ya kutoa posa yamekuja baada ya kuona kila mmoja anaweza kuishi na mwingine kwani wameshasomana kwa muda mrefu.
“Najua si jambo la watu kuhoji sana kwa sababu ndoa ipo na kila mtu atafanya hivyo, nina hela ya mahari tayari na siku ikipangwa ya kutoa tutafanya hivyo lakini ninachowaza sasa ni kuona nafanya vipi ili harusi yangu iwe ya kipekee na zoezi hili tutalifanya mwakani,” alisema.

MWANAMKE ADAIWA KUTEKA WATOTO
Stori: Shani Ramadhani
Mama mmoja, Sara Zoya mkazi wa Mabibo Makuburi, jijini Dar es Salaam amekimbilia polisi na kudai kuwa watoto wake walitekwa na ndugu yake kisha kupelekwa kusikojulikana baada ya kufukuzwa kwenye nyumba yao ya familia.

Monday, December 29, 2014
The Carters walivyo sheherekea Birthday Ya Jay Z
Ni kweli Beyonce anajua kumfanya Jay Z awe mtu mwenye raha sasa kama
inavyonyesha kwenye baadhi ya picha walizopiga kwenye siku ya kuzaliwa
ya Jay Z ‘Dec 4′ . Wawili hawa walikwenda Iceland kujiachia kwa muda
huku wakisherehekea miaka 45 ya maisha ya Jay Z

JACK PATRICK ATWANGWA TALAKA AKIWA JELA
Masikini! Wakati akiendelea kutumikia kifungo cha
miaka saba jela huko Macau nchini China, mwanamitindo mwenye mvuto wa
kipekee Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick, ametwangwa
talaka na aliyekuwa mumewe, Abdullatif Fundikira ‘Tiff’ na tayari
amemuoa Miss Tanzania 2011, Salha Israel.

Wakati mwanamitindo Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick akiwa na mumewe, Abdullatif Fundikira ‘Tiff’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda wikiendi iliyopita baada ya gazeti
ndugu na hili, Amani kutoa habari ya Miss Tanzania kuolewa na mume wa
Jack, Tiff alisema kuwa mke wake wa sasa (Salha) amemuoa kihalali na
kwamba yeye siyo mume wa mtu kwa sababu ameshampa talaka Jack aliyemuoa
mwaka 2011.ROSE MUHANDO KWA UTAPELI TOO MUCH!
LILE jinamizi la kupokea
fedha kwa ajili ya kushiriki tamasha la kuimba nyimbo za Injili kisha
kutotokea siku ya tukio linazidi kumwandama nyota wa muziki huo nchini,
Rose Athuman Muhando, safari hii akidaiwa kumliza tena mtu, Ijumaa
Wikienda lina kesi hiyo mkononi.
Nyota wa muziki huo nchini, Rose Athuman Muhando.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha ndani, safari hii ameendelea kupokea
fedha kutoka kwa mshirika wake kwenye mambo ya Injili, Alex Msama kwa
makubaliano ya kushiriki Tamasha la Krismasi kwenye Uwanja wa Samora
mjini Iringa lakini siku ya tukio, Ijumaa iliyopita, mwanadada huyo
hakutokea!BATULI: NAYACHUKIA MAPENZI YALIYOPITA

STAA mkali wa filamu za hapa Bongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amefunguka kuwa hakuna kitu ambacho kinamuuza na kukichukia kama mapenzi yaliyopita.
Staa mkali wa filamu za hapa Bongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Batuli alisema
kuwa anachukia na kudharau mno uhusiano uliopita kwani haukuwa ni sahii
kwake hivyo hataki hata kuukumbuka.“Nayachukia sana mapenzi yaliyopita kwa kweli na kuna wakati sipendi kabisa kuifanya akili yangu ikumbuke uhusiano wa nyuma, maana hauna kumbukumbu nzuri kwangu,” alisema Batuli ambaye alishawahi kubanjuka penzini na mwigizaji Mohamed Mtonesia ‘Mtunis’ na Mr. Kelvin walifunga naye ndoa na kumwagana.
DUDE: MWAKA 2014 NI GUNDU KWANGU

TUKIWA tunaelekea ukingoni mwa mwaka, msanii wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amefunguka kuwa mwaka 2014 ulikuwa hauna bahati (gundu) hivyo anamuomba Mungu huo ujao uwe wa baraka kwake.
Msanii wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Akipiga stori na gazeti hili, Dude alisema ndani ya mwaka huu
hakuweza kufanikisha lengo lolote kati ya yale aliyojiwekea ikiwa ni
pamoja na kufunga ndoa jambo ambalo linamuumiza kwani alitegemea kufanya
mambo mengi lakini hakufanikisha.“Nilitegemea kufunga ndoa lakini imeshindikana kwa sababu upande wa kazi mambo hayakuwa mazuri pia nilipanga kwamba kipindi changu cha Bongo Dar es Salaam kitarudi hewani lakini ikashindikana, ukweli mwaka huu haukuwa mzuri kabisa kwangu namuomba Mungu ujao akanifanikishe malengo yangu,” alisema Dude.
Saturday, December 27, 2014
BABY MADAHA MAPENZI NI HOBI YANGU
Mwanadada asiyeishiwa matukio Bongo, Baby Madaha.
Stori: Gladness Mallya MWANADADA
asiyeishiwa matukio Bongo, Baby Madaha ameibuka na kutoa kali ya mwaka
kwamba anapenda mapenzi kuliko kitu kingine chochote duniani.DIAMOND HANA UWEZO WA KUMPA MWANAMKE UJAUZOTO!
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Penny.
BAADA ya kudaiwa na staa
wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa alichoropoa mimba
zake mbili, mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’ ameibuka
na kujibu mapigo kwamba mwanamuziki huyo hana uwezo wa kumpa mwanamke
mimba, Risasi Jumamosi linakupa mchapo kamili.
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Wema Sepetu.
CHANZO CHA YOTEAkizungumza na GlobalTV Online kwenye ofisi za gazeti hili Bamaga-Mwenge jijini Dar, hivi karibuni, Diamond alifunguka: “Nilimpa (Penny) mimba ya kwanza, sikuamini ikabidi twende naye hospitalini tukapime, akaambiwa anayo…nikafurahi nikampiga na ndinga (gari) mpya siku hiyohiyo, nikamwambia mama tulia unizalie mwanangu.
WASTARA KUMUANIKA MRITHI WA SAJUKI
Staa wa filamu Bongo, Wastara Juma.
Stori: Imelda Mtema STAA wa
filamu Bongo, Wastara Juma, ametamka hadharani kuwa hana uhusiano wa
kimapenzi na msanii yeyote ndani ya Kundi la Bongo Movie.Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Wastara alisema kuna maneno mengi yanasemwa kuwa ana uhusiano na mtu ndani ya kundi hilo kitu ambacho si sahihi, atamuanika mrithi wa marehemu Sajuki siku si nyingi.
“Unajua muda utafika tu lakini kwa hivi sasa sina bwana wala sihitaji mtu yeyote ndani ya Kundi la Bongo Movie na mtu ambaye ataishi na mimi muda ukifika nitawatambulisha na kila mmoja atamjua na siyo mtu kunitabiria au kubuni nitamuweka wazi muda si mrefu,” alisema Wastara.
MTOTO ASOMBWA NA MAJI, AFARIKI

CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
MTOTO wa miaka sita, Bernard Benjamin ambaye alikuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Nyamunge, wilayani Ilemela jijini Mwanza, amesombwa na mafuriko na mwili wake kukaa siku kumi na tano bila kuharibika.
Mafuriko yaliyosababisha kifo cha marehemu mtoto Bernard Benjamin.
Tukio hilo lilijiri Desemba 2, mwaka huu kwenye Mto Kenge jijini
hapa, maeneo ya Mabatini, Wilaya ya Nyamagana baada ya kujaa maji ambapo
marehemu alisombwa na mafuriko hadi pembezoni mwa Ziwa Victoria.Friday, December 26, 2014
SAFARI YA MABALOZI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KATIKA SIKU YA KWANZA
TAMASHA LA WAFALME: MZEE YUSUF AFANYA KWELI, NYOMI YAPAGAWA DAR LIVE
SHOO YA DIAMOND DAR LIVE YAACHA HISTORIA
R.I.P WASANII WETU! KINACHOWAUA KWA KASI CHAJULIKANA

Inauma sana! Katika kipindi cha miaka mitatu kuwapoteza wasanii kwa kiasi hicho ni pigo kubwa kwa tasnia, hasa filamu na muziki, ukiwemo wa muziki wa Injili.
Leo katika toleo hili maalum, Ijumaa linawakumbusha wasanii hao walioaga dunia na namna vifo vyao vilivyotokea.
Leo katika toleo hili maalum, Ijumaa linawakumbusha wasanii hao walioaga dunia na namna vifo vyao vilivyotokea.
ALBERT MANGWEHA ‘NGEA’
Alikuwa msanii wa Bongo Fleva. Akiwa na miaka 31 alifariki dunia Mei 28, 2013 nchini Afrika Kusini. Chanzo cha kifo chake inadaiwa ni matumizi yaliyopitiliza ya madawa ya kulevya. Alizikwa Morogoro, Tanzania, Juni 6, 2013.

LANGA KILEO ‘RAIS WA GHETO’
Alikuwa msanii wa Bongo Fleva. Alifariki dunia Juni 13, 2013 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar akiwa na miaka 28. Kifo chake kilithibitishwa kuwa, kilitokana na kuzidiwa na Ugonjwa wa Malaria. Alizikwa Juni 17, kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.

Thursday, December 25, 2014
Nicki Minaj Kwenye Kurasa Ya Mbele Ya Jarida La Rolling Stone

Kwenye chati kubwa za dunia za album, Nicki Minaj amefanikiwa kushika na 2 kwenye wiki ya kwanza ya kutoka kwa album yake ya Pink Print ikikadiriwa kuuza kopi 150,000 na mpaka sasa imeuza kopi 244,000 .

MADAI MAZITO ROSE NDAUKA, RICHIE WARUDIANA
Na Waandishi Wetu
MASTAA wa sinema waliowahi kuwa wapenzi enzi hizo, Rose Ndauka na Single Mtambalike ‘Richie’ wanadaiwa kurudiana na hivi sasa ni mapenzi motomoto!Kwa mujibu wa chanzo, Rose na Richie wamedaiwa kurudiana baada ya mwanadada huyo kumwagana na mzazi mwenzake, Malick Bandawe miezi ya hivi karibuni.

MARTIN KADINDA KUOA SOON!
Na Laurent Samatta
MBUNIFU wa mavazi Bongo, Martin Kadinda, amesema kuwa baada ya kuishi bachela kwa miaka mingi amepanga kuoa ‘ soon’ mwanamke ambaye ni mpenzi wake wa siku nyingi ili kumaliza maneno ya watu kuwa hajiwezi.
Akizungumza na Amani, Kadinda alisema kuwa mwanamke anayemuoa si aliyezaa naye mtoto bali ni mwanamke aliyekuwa naye kwenye uhusiano kwa muda mrefu na tayari anatambua tabia zake hivyo hana shaka juu ya kuishi kwao pamoja.
“Wazazi wako tayari juu ya hilo nadhani na sitaki kumweka hadharani sasa hivi maana watu hawakawii kuharibu kwa maneno yao machafu, lakini wale ambao walidhani sitaweza kufanya hivyo watambue kuwa mwakani naoa,” alisema Kadinda.
ESCROW BADO MOTO
WAKATI Rais Jakaya Kikwete akiwa amemuwajibisha
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka kufuatia
kumegewa mgawo wa fedha za Tegeta Escrow, binti anayedaiwa kuwa mwanaye,
amejikuta akipata wakati mgumu baada ya kumtetea mama yake kupitia
mitandao ya kijamii.
Katika Mtandao wa Twitter, binti huyo aliyejitambulisha kwa jina la Kagem Tibaijuka, alimtetea mama yake akisema fedha zilizowekwa kwenye akaunti yake zilikuwa ni safi na halali na kwamba ziliwekwa kwa nia njema ya kuwasaidia kielimu watoto wa kike.
“My mum did nothing wrong except wanting to help young girls get an education. A school built with my late father. Accepted a donation,” (Mama yangu hakufanya kosa lolote isipokuwa alitaka kuwasaidia wasichana kupata elimu. Shule ilijengwa na marehemu baba yangu. Mchango ukakubaliwa)yalikuwa ni moja ya maneno yake katika mtandao huo wa Twitter.
Aidha, aliwashambulia wanawake walioonekana kushangilia wakati Rais Kikwete alipotangaza kumuwajibisha mama yake, akiwaambia kuwa anawashangaa kushangilia anguko la mwanamke mwenzao na kwamba hata wao iko siku yatawakuta ya kuwakuta.
Lakini katika mitandao mingine ya kijamii, ikiwemo Facebook na Jamii Forum inayotembelewa na watanzania wengi, walimshambulia binti huyo kwa kumwelezea kama mtu aliyelewa fedha na kwamba mama yake alistahili kuondolewa kwenye nafasi yake, ikiwa ni pamoja na kushtakiwa.

HUKU MKEWE AKISOTA GEREZANI MISS TZ AOLEWA NA MUME WA JACK PATRICK

Kwa mujibu wa chanzo makini, uhusiano wa Salha na Tif uliibuka na kushamiri mwaka jana baada ya Jack kukamatwa na unga huo.“Penzi lao liliibuka ghafla tu, jamaa naona ana ‘aleji’ na warembo wenye majina yao maana penzi lake na Jack lilipoyumba na kisha mrembo huyo kukamatwa na madawa ya kulevya nchini China, fasta akaanzisha uhusiano na Salha,” kilisema chanzo hicho.
UMAARUFU WA JACK UPOJE?
Jack ni mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2006 akitokea Miss Ilala lakini umaarufu wake ulizidi kukua baada ya kushiriki kama ‘video queen’ katika video mbalimbali za wasanii wa muziki wa Bongo Fleva ikiwemo video ya She Got Gwan ya marehemu Albert Mangwea.
Miss Tanzania 2011, Salha Israel akipozi.
VYANZO VINGINEHata hivyo, vyanzo vingine vimeeleza kuwa, Jack na mumewe walikuwa na mgogoro mzito kabla modo huyo hajakamatwa na madawa ya kulevya.“Walikuwa na mgogoro, ilifika wakati Jack alikuwa akidai talaka mahakamani lakini bahati mbaya kabla hajafanikiwa kupewa akaswekwa nyuma ya ndondo,” kilieleza chanzo hicho.