BAADA ya wiki iliyopita msanii wa filamu Bongo,
Wastara Juma kuripotiwa kwenye moja ya magazeti pendwa kuwa hana
uhusiano na mtu yeyote ndani ya Bongo Muvi na yupo mbioni kumuanika
mrithi wa Sajuki mengi yameendelea kuibuka.
Akizungumza na Uwazi, mpenzi wa Wastara anayetambulika kwa jina la
Bondi Bin Salim alidai kuwa yupo kwenye mchakato wa mwisho wa kutoa
mahari kwa ndugu wa msanii huyo kiasi cha shilingi milioni 5 pamoja na
pete za dhahabu ili aweze kuwa na Wastara.
Alisema kuwa maamuzi ya kutoa posa yamekuja baada ya kuona kila mmoja
anaweza kuishi na mwingine kwani wameshasomana kwa muda mrefu.
“Najua si jambo la watu kuhoji sana kwa sababu ndoa ipo na kila mtu
atafanya hivyo, nina hela ya mahari tayari na siku ikipangwa ya kutoa
tutafanya hivyo lakini ninachowaza sasa ni kuona nafanya vipi ili harusi
yangu iwe ya kipekee na zoezi hili tutalifanya mwakani,” alisema.
No comments:
Post a Comment