Msanii wa filamu Bongo, Flora Mvungi ‘H-Mama’.
Stori:Chande Abdallah Msanii wa filamu Bongo,
Flora Mvungi ‘H-Mama’ amewashinikiza wasanii wenzake wa kike kuzaa
mapema huku akiwataka kuingia kwenye hatua ya kuitwa mama na kusema
kuzaa kuna raha yake.
Akizungumza na mwandishi wetu, Flora alisema baadhi ya mastaa
wamekuwa na dhana potofu kwamba, ukizaa unazeeka na utakuwa hufanyi
starehe, jambo ambalo halina ukweli.
“Mimi nawashauri wazae tu, kuzaa kuna raha yake bwana. Unajua starehe
haziishi, kikubwa ni wao kuzaa fasta kisha mambo mengine yanaendelea
huku tayari wakiwa wameshaweka ile heshima ya kuitwa mama,” alisema
Flora.
No comments:
Post a Comment