HII ni ‘bad news’ kwa staa namba moja wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’. Mfanyabiashara maarufu nchini Uganda anayefahamika
kwa jina la King Lawrence, ameibuka na kumuita nyota huyo shoga.
ISHU ILIPOIBUKIA
King ambaye ana makazi yake pia
nchini Afrika Kusini, amedaiwa kutoa kauli hiyo juzi, Jumatano kupitia
mtandao wa Facebook akionesha kukerwa na kitendo cha staa wa muziki
Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’ kuangukia katika penzi la Diamond.
ATUMIA GIA YA WATOTO
Awali, King ambaye
imeelezwa alikuwa na urafiki na dereva wa aliyekuwa mume wa Zari, Ivan
Semwanga, alianza kwa kumchokonoa Diamond kwa gia ya kujifanya
anawatetea watoto wa Zari ambapo alitupia picha ya Zari akiwa na Diamond
mtandaoni ikiwa na ujumbe wenye kejeli na jeuri ya fedha.
UJUMBE ULIVYOSOMEKA
“As a concerned uncle, Im
offering Zari’s tomboy Diamond Dola 40,000 so as to leave the old mom of
three to take care of her kids. The young boys miss their mom. Please
Diamond do it for the kids.”
(Nikiwa kama mjomba, ninampa jikedume
wa Zari, Diamond, Dola 40, 000 (Sh. Mil 66) ili amuache mama wa watoto
watatu (Zari) awalee vizuri watoto wake. Watoto wanammisi mama yao.”
ABADILISHA GIA
Kuonesha ana mpango mchafu wa
kumchafua Diamond ambaye anaipeperusha vyema bendera ya Afrika kimuziki,
badala ya ishu ya watoto, alibadili upepo na kujinadi eti yeye ndiye wa
kwanza kutembea na Zari.
Pasipo kueleweka kusudi lake, alimpiga
dongo Diamond ambaye usiku wa kuamkia leo alipewa heshima ya kipekee
kutumbuiza kwenye Tuzo za Wanamichezo Bora zilizoandaliwa na Shirikisho
la Afrika (Caf) nchini Nigeria.
HEBU MSIKIE
“Kwa nini utembee na Diamond shoga? Sijui kama anajua kwamba mimi ndiyo
wa kwanza kutembea na wewe (Zari),” aliandika katika mtandao wa
Facebook.
AZIDI KUTAPATAPA
Kama hiyo
haitoshi, kupitia mtandao wa Facebook, King alitupia mawasiliano yake ya
zamani na Zari akidai alikuwa akimuomba fedha.
DIAMOND ANASEMAJE?
Hadi tunakwenda mitamboni,
jitihada za kumpata Diamond ili aweze kujibu tuhuma hizo hazikuzaa
matunda huenda ni kutokana na ubize aliokuwa nao katika maandalizi ya
shoo hiyo kubwa Afrika, simu yake iliita bila kupokelewa na hata
alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu.
ZARI AMSAFISHA DIAMOND
Kupitia mtandao huo, Zari
naye aliibuka na kumtetea Diamond akimwambia King ana chuki binafsi
kwani hapendi kumuona akiwa na furaha.
“Hatuna muda wa kukujadili, unafikiri Diamond anaweza kuwa shoga?
Unafikiri anaweza kubishana na wewe? Kweli nimeamini, watu wakikuona una
furaha, wanaanza kukuchukia,” alijibu Zari maneno hayo ambayo pia
ameyaweka katika akaunti yake ya mtandao wa Instagram.
DIAMOND NI SHOGA?
Kutokana na madai hayo ya
King, baadhi ya wadau wakubwa wa muziki Bongo walikanusha vikali madai
hayo kwa kudai jamaa huyo ana lengo la kumchafua Diamond kwa kuwa kwa
sasa anafanya vizuri Afrika nzima.
“Hana lolote huyo King, anatafuta
kiki za kipuuzi, atamuitaje Diamond shoga? Amewahi kumuona akifanya
vitendo hivyo? Wivu tu wa maendeleo, aache Diamond na Zari wafanye yao,
apeperushe muziki wetu nje ya Afrika,” alisema mdau mmoja ambaye
hakupenda jina lake liandikwe gazetini.
KING ANATESWA NA WIVU?
Licha ya awali King
kutoonesha kwamba aliwahi kutembea na Zari, katika maelezo yake ya pili
yameonesha dhahiri kwamba anasumbuliwa na wivu wa mapenzi kutokana na
kujinadi kuwa yeye alikuwa wa kwanza kutembea na Zari.
“We huoni
ameanza kwa kujifanya anawatetea watoto, mara akajifanya rafiki wa
dereva wa Ivan mara tena amegeuka anadai alikuwa wa kwanza kutembea na
Zari hana lolote wivu tu unamsumbua atakuwa alimtaka mtoto mzuri
akamchomolea,” aliandika mdau mmoja katika mtandao wa Instagram.
KING NI NANI?
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali,
jamaa huyo ni mfanyabiashara maarufu nchini Uganda na Afrika Kusini na
amekuwa akijinasibu kuwa na uhusiano na mastaa mbalimbali wa Uganda
akiwemo mwanamuziki Julia Kanyomozi.
No comments:
Post a Comment