MASTAA wa filamu ya Daddy’s Wedding, Yvone Sheryl
‘Monalisa’, Banana Zoro, Sandra, Mama Abdul na wenzao hivi karibuni
walipata ajali walipokuwa kwenye maandalizi ya filamu hiyo kwenye mbuga
ya Saadani.
Ajali hiyo ilitokea katika daraja moja dogo mbugani hapo ambapo
walikusanyika kwa ajili ya kushuti mojawapo ya vipande vya filamu hiyo
mpya, lakini likaporomoka na kuwafanya baadhi yao kuumia na wengine
kupata mshtuko mkubwa.
“Aliyeumia zaidi ni Sandra lakini alipewa matibabu ya haraka na
kuruhusiwa, ila tunamshukuru Mungu tulifanikiwa kumaliza salama na
hatukudaiwa chochote,” alisema na kumtaja pia Jenerali Ulimwengu kuwa
mmoja kati ya waigizaji walio ndani ya filamu hiyo.
No comments:
Post a Comment