MSANII mkongwe katika filamu Bongo, Salome Urassa
‘Thea’ amefunguka na kusema kwamba kwa sasa amebadili aina ya maisha
yake kwa kuwaepuka marafiki wanafiki aliokuwa akikutana nao kwenye
makundi ya majungu.
Akipiga stori mbili tatu na gazeti hili hivi karibuni, Thea alisema
siku hizi hata akienda location anafanya kile kilichompeleka na baada
ya hapo anarudi nyumbani mapema ili kumuwahi mumewe.
“Siku hizi nikienda location nafanya kilichonipeleka, nabadilisha
nguo narudi nyumbani kwangu maana sipendi sana kukaa kwenye vikao yaani
makundi maana ndiyo mwanzo wa manenomaneno na majungu hivyo nayaepuka,
kwani hayanisaidii pia nimepunguza marafiki maana mimi ni mke wa mtu,”
alisema Thea.
No comments:
Post a Comment