STAA wa filamu Bongo, Shamsa Ford amefungukia
uhusiano wake kwa mara ya kwanza na mumewe, Dickson Matoke kwamba
walikutana kiajabuajabu na kuwa wapenzi.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Kipindi cha Me and You With
Love kilichofanywa na Global TV hivi karibuni, Shamsa alisema kuwa siku
ya kwanza hakudhani kama Dick ndiye atakuwa mumewe kwani walikuwa
wakikutana katika kumbi za starehe tu.
“Siku ya kwanza tulibadilishana namba na ukawa ndiyo kama mchezo,
kila tukitaka kwenda kwenye starehe alikuwa akinipigia simu hadi ikawa
mazoea na kujikuta tukiangukia katika penzi,” alisema Shamsa.
Shamsa
ameongea mengi kuhusiana na mapenzi na maisha yake kwa ujumla.
Mahojiano kamili yatapatikana Alhamisi ya wiki hii kupitia www.globaltvtz.com
No comments:
Post a Comment