Ugonjwa unaowakabili watoto waliotoka mgongo nje pamoja na vichwa
vikubwa, unaelezwa kusababishwa na ukosefu wa Folic Acid mwilini, hali
inayochangiwa na mama mjamzito kupenda kula chipsi kuku.Daktari wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wodi ya watoto ya Moi, Agricore Joseph
alisema wanawake wengi hufikia hatua ya kujifungua watoto wenye matatizo
hayo kutokana na kupenda vyakula hivyo, kitu ambacho kinaweza
kuepukika.
Dokta Agricore aliyasema hayo alipokutana na MC maarufu jijini Dar,
Joyce Amina Mwakipunda ‘Mc Jojo’ na Mtangazaji wa Kipindi cha Tashtiti
Zetu cha Redio Uhuru, Nuru Issa, walipofika hospitalini hapo kutoa
misaada mbalimbali kama vile pampasi, mafuta, poda, maji ya kunywa,
juisi ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku yao ya kuzaliwa.
“Nakujua wewe ni MC maarufu, huko unakopita jaribu kuwaelimisha
wanawake juu ya tatizo hilo, na wewe Nuru kwenye kile kipindi chako
waelimishe wanawake juu ya hili, naamimi tunaweza kupunguza idadi ya
wanaojifungua watoto wenye tatizo hili,” alisema daktari huyo.Alisema,
ni wakati sasa wanawake hasa wajawazito kuelimishwa juu ya kutopendelea
chipsi kuku badala yake kutumia vyakula ambavyo vinaongeza Folic Acid na
kunywa vidonge vinavyotolewa kliniki.
No comments:
Post a Comment