KIMENUKA! MKEwa staa wa sinema za Kibongo, Jimmy
Mafufu, Salma Sadiki amenaswa akifungasha virago nyumbani kwake
Mwananyamala-Hospitali na kuelekea kwa wazazi wake maeneo ya Mbagala
jijini Dar akidai kuchoshwa na tabia za mumewe huyo, Ijumaa lina ‘full’
stori.
Akizungumza na mapaparazi wetu, Salma alisema kwa kipindi kirefu
msanii huyo amekuwa akimuonyesha tabia za ajabu ikiwemo hivi karibuni
kunaswa akiwa amezungukwa na vimwana kana kwamba si mume wa mtu.“Mara
nyingi akiwa anatoka kwenye shughuli za usiku huwa tunatoka wote lakini
cha ajabu kuna siku alinigomea kabisa kwenda naye kwenye lile onesho la
Twanga Pepeta, akarudi saa 11 alfajiri na kwenye bethidei ya mtoto wa
Davina akaniambia mimi nibaki nyumbani kumbe alikuwa ana mambo yake huko
kwani alirudi asubuhi saa 12.
“Nimevumilia mengi sana kwenye hii ndoa mpaka leo kuamua kuondoka.
Acha nimuache na mambo yake,” alisema Salma kwa masikitiko.Alisema japo
katika uhusiano wao wana miaka isiyopungua saba, walikuwa kwenye uchumba
kwa miaka minne na baadaye wakafunga ndoa mwaka 2013 lakini anashindwa
kukumbuka alipotoka.
Baada ya kushuhudia Salma akiondoka nyumbani hapo, mapaparazi wetu
walimtafuta Jimmy kwa njia ya simu ili kumsikia anazungumziaje madai ya
mkewe ambapo alisema mkewe huyo amekuwa akimuonea wivu usiokuwa na
maana.
“Mke wangu nampenda sana na tangu nimuoe sijawahi kumsaliti sema tu
anakosa imani kwa mambo madogo sana. Kama mwenyewe kaamua kuondoka
kutokana na wivu wake mimi siwezi kumfuata,” alisema Mafufu.
No comments:
Post a Comment