Msanii wa muziki, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, ameeleza kuwa
endapo msanii mwenzake ambaye sasa hivi wanapika na kupakua, Shamsa Ford
atamuonesha utulivu na uaminifu hataona sababu ya kutomuoa.
Nay aliyasema hayo juzikati alipokuwa akizungumzia mipango yake na
Shamsa ambaye amejiweka kwake baada ya kutosana na mzazi mwenzake,
Siwema. Nay alisema: “Hilo la ndoa kiukweli kabisa kama Shamsa ataonesha
kutulia na kunithibitishia kuwa hatakuja kunizungua, sitaona hatari
kumuoa.”
No comments:
Post a Comment