Mshiriki wa Bongo Star Search (BSS), mwaka 2010/2011, Bella Kombo.
Shani ramadhani
MSHIRIKI wa
Bongo Star Search (BSS), mwaka 2010/2011, Bella Kombo ameweka wazi kuwa
sasa hivi ameamua kumtumikia Mungu na kuachana na muziki wa kidunia
aliokuwa akiufanya awali.
Akipiga stori na Amani, Bella alisema baada ya Shindano la BSS
alikuwa anaimba katika bendi na pia ameshafanya kolabo na wasanii kama
Hemed Phd, Tunda Man, Kala Jeremiah, Steve RnB, lakini mwaka jana
aliamua kurudi rasmi kwenye nyimbo za Injili.
“Nimekulia kwenye familia ya watu waliookoka kwa hiyo sijaanza
kuokoka hivi karibuni ni malezi ambayo nimekuwa nayo tangu nimezaliwa na
ninayaendeleza mpaka sasa, niko kwenye maandalizi ya kutoa albamu yangu
ya nyimbo za Injili,” alisema Bella.
No comments:
Post a Comment