MUIGIZAJI mwenye mvuto anayekuja kasi katika tasnia
ya filamu Bongo, Ester Kiama ameweka bayana kuwa hapendi kuwa na
marafiki wa kike na hana.
Akifunguka kiunagaubaga, Ester alisema kutokana na malezi na maisha
yalivyo sasa inabidi aepuke marafiki ambao wengi wao ni wanafiki.
“Wengi wanajua naringa sana lakini ukweli sipo hivyo ndiyo maana muda
mwingi nautumia katika kufanya shughuli zangu na kujiepusha na makundi
kwani najua madhara yake, washikaji zangu ni wanaume kwani najifunza
mengi kupitia kwao,” alisema Ester.
No comments:
Post a Comment