Pages

Wednesday, November 7, 2012

ISHA MASHAUZI, BANANA ZORRO MAMBO HADHARANI.

MWIMBAJI na mkurugenzi wa kundi la Mashauzi Classic, Isha Ramadhan na mkurugenzi wa B-Band, Banana Zorro hatimae wamefichua siri ya ukaribu wao.
Wakali hao wamesema ukaribu wao wa hivi karibuni ulikuwa ni wa kutengeneza wimbo wa Bongo Fleva waliouimba kwa pamoja ambao umepewa jina la “Ukinipenda”. CHANZO CHA HBARI SALUTI5(www.saluti5.com).
Wimbo huo ambao ulirekodiwa hivi karibuni kupitia studio za FishCrab chini ya Lamar tayari umeanza kusambazwa kwenye vituo vya redio, huku maandalizi ya video yake yakiwa ukingoni kupitia studio hizo hizo za FishCrab.
Isha ambaye ameonyesha uwezo mkubwa katika kazi hiyo aliiambia Saluti5.com kuwa kukamilika kwa wimbo huo ndio mwanzo wa matayarisho ya nyimbo zingine ili kukamilisha albam yake ya kwanza ya miondoko ya Bongo Fleva ambayo itakuwa na jumla ya nyimbo 6.
Aidha Isha alisema katika albam hiyo atashirikisha wasanii wengine katika baadhi ya nyimbo na zingine ataimba yeye peke yake.

No comments:

Post a Comment